Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (katikati) akiongoza kikao cha majadiliano juu ya ushirikiano na Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) wakati uongozi wa Chuo hicho walipotembelea Ofisi za TADB. Msafara wa huo wa Chuo cha Kilimo uliongozwa na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Susan Nchimbi-Msolla (wapili kulia) na msaidizi wake Prof. Benard Chove (kulia). Wengine pichani ni wajumbe wa menejimenti ya TADB.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kushoto) akibadilishana hati za makubaliano na Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Susan Nchimbi-Msolla. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Sheria na Huduma wa TADB, Bibi Neema-Christina John (Kushotot) na Naibu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Benard Chove (kulia). Makubaliano hayo yalisainiwa katika Ofisi za TADB, Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kushoto) and Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Susan Nchimbi-Msolla wakionesha hati za makubaliano. Makubaliano hayo yanalenga uendelezaji wa masuala ya utafiti na kujengea uwezo wa kitaasisi baina ya pande hizo mbili. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Sheria na Huduma wa TADB, Bibi Neema-Christina John (Kushoto) na Naibu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Benard Chove (kulia).