Polisi katika mji wa Manchester nchini Uingereza wanasema watu 22 wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa kwenye mulipuko uliotokea ndani ya ukumbi wa tamasha la muziki.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi.
Ikiwa itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50 walikufa kwenye misururu ya milipuko mjini London.
Manchester explosionHaki miliki ya pichaPETER BYRNE
Image captionWatu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza
Watu walioshuhudia mulipuko huo wa Manchester wamesema mwamziki wa Marekani Ariana Grande alikua amemaliza kuwatumbuiza mashabiki wake, wakati mulipuko mkubwa ulisikika na kutikisa ukumbi mzima.
Mashahidi wamesema kuona misumari iliyotapakaa sakafuni na harufu ya vilipuzi.
Manchester explosionHaki miliki ya pichaPETER BYRNE
Image captionWatu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza
Eneo kulikotokea mulipuko huo limezingirwa na polisi waliojihami wanaendelea kushika doria.
Wakati huo huo Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo.
Manchester terror attackHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza
Ripoti ambazo hazijathitishwa kutoka kwa maafisa wa Marekani ambao hawakutajawa zinasema kuwa shambulizi hilo lilifanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga.
Manchester explosionHaki miliki ya pichaPETER BYRNE
Ukumbi wa Manchester ambao ulikuwa ukifahamika awali kama ukumbi wa wanaume, ndio ukumbua mkubwa zaidi mjini humo wenye uwezo wa kuwachukua watu 18,000
Barabara ya ukumbi huo unuangana na kituoacha treni cha Victoria kati kati mwa mji.
Manchester explosionHaki miliki ya pichaPETER BYRNE
Image captionWatu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza
Ukumbi huo hutumiwa kuandaa tamasha za manyota wakuu kama Ariana Grande nyota wa runinga mwenye umri wa miaka 23 ambaye sasa ni nyota wa muziki wa pop.
Manchester terror attackHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWatu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza
Manchester explosionHaki miliki ya pichaPAUL ELLIS
Image captionWatu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza