picha na maktaba

Kikosi cha Afc
Arusha kimejinasibu kuwa kitawafunga mabigwa wa ligi kuu bara msimu
uliomalizika  Timu ya  Yanga Afrika,katika mchezo wao wa kirafiki
unaotajarajiwa kupichezwa Jumapili hii
May 28 katika kiwanja cha kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa






Akiongea na gazeti hili kocha wa kikosi hichi kipya cha timu
ya AFC Fikiri Elias  alisema kuwa vijana
wake wapo tayari kuwapatia burudani wapenzi wa ke wa soka mkoani hapa huku
akiwapa sifa viongozi wa serikali kwa kuwa begakwa bega katika kuhakikisha soka
la mkoa wa Arusha linarudi katika ramani yake




Alisema kuwa japo hii ni mechi yao ya kirafiki baina yao na
timu ya Yanga lakini watatumia mchezo huu pia kuangalia kikosi bora ambacho
kitakaa kambini kwa ajili ya kuandaa timu ya kikosi kitakacho unda AFC mpya
itayoshiriki ligi daraja la kwanza .





,, pamoja ya kuwa timu ya yanga inawachezaji wazoefu wengi
na pia ndio wametoka tu kutwaa ubigwa mara ya tatu lakini napenda kusema hivi
japo mechi hii ni ya kirafiki lakini nimeaada kikosi kizuri nanauhakika lazima
tutaifunga timu hii ili tuweke historia japo ni mechi ya kirafiki ,,alisema
Fikiri









Kwa upande wake kocha msaidizi  timu ya
Yanga ambao wameshikilia ubigwa  kwa mara ya tatu mfulukizo ligi kuu bara  Juma Mwambusi alisema kuwa mchezo huu ni
muhimu  kwao kwani ni moja  ya program zao katika kujiandaa kuelekea
katika michuzano inayowakabili  ikiwemo
mashindano ya Sport Pesa





Kikosi hichi cha yanga kipo katika ziara ya kutembeza kombe
lake kwa mashabiki wa mikoani ambapo mkoa wa Arusha umekuwa wa kwanza kuona
kombe hilo na wakitoka mkoani hapa wanampango wa kulipeleka mkoani Dodoma
,ambapo pia wanajangwan hawa wamekuwa ni timu ya tatu kuoka ligi kuu bara msimu
ulioisha kutoa katika aridhi ya jiji la Arusha iliyokuwa na ukame wa timu za
ligi kuu mara baada ya timu za Ruvu shooting na Simba  zilizowaikutua hapa katika mtanange wake
ulioisha









Akizungumzia mchezo huo wa kirafiki  mmoja wawaandaaji wa mechi hiyo ambayo katibu
wa timu ya AFC  Charles Mwaimu alisema
kuwa maandalizi yote yamekamilika timu zote zipo tayari wanaisubiri tu siku ya
mechi ifike.









Aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha na pembezoni kujitokeza
kwa wingi kuishabikia timuyao ya AFC ikiwa ni ujio mpya wa timu hii mara baada
ya kupotea kwa muda ,na aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kuwapa
morali wachezaji wao .









Aidha alisema kuwa pia mbali na mechi hii ya yanga kucheza
na AFC pia wanampango wa timu hii kwenda mkoani manyara kucheza mechi baida yao
na timui ya Merirani.

Na Woinde Shizza,Arusha