Rais wa shirikisho la kandanda nchini Tanzania (TFF) Jamal Malizia, amekamatwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini humo.
Alikamatwa pamoja na katibu wa TFF Selestine Mwesigwa.

Wawili hao walizuiliwa usiku kucha.
Msemaji wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Musa Misalaba aliongeza kuwa wawili hao watabaki kizuizini hadi wahojiwe.
Kukamatwa kwao kunajiri baada ya uchunguzi wa siku nyingi.
Misalaba alisema kuwa idara hiyo inaendelea kuwachunguza maafisa waengine kwa madai sawa na hayo.