Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 12, 2017

WAKAZI WA MANISPAA YA UBUNGO WAMPONGEZA JPM KWA MAAMUZI MAGUMU KWA MANUFAA YA WATANZANIARais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli


Wakazi wa Mitaa tofauti tofauti katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es
salaam ukiwemo Mtaa wa kimara, Ubungo, Sinza, Mabibo, Mwembechai na Magomeni
wamempongeza Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli
kwa kuunga mkono maoni/Mapendekezo ya Ripoti ya pili ya wachumi na wanasheria
iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo kwenye makontena zaidi 250 yenye mchanga
wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani
ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam.
Rais
Magufuli ameunga mkono ripoti hiyo kutokana na ukiukwaji wa sheria za nchi na upotevu
mkubwa wa mapato ya Serikali kupitia biashara ya Makinikia na madini
yanayosafirishwa nje ya nchi.
Wananchi
hao wamesifu uwepo wa Rais Magufuli huku wakieleza kuwa Tanzania imefanikiwa
kupata kiongozi imara na madhubuti atakayeweza kuifanya Tanzania kuwa ya neema
na mafanuikio makubwa.
Mapendekezo
hayo ya kamati maalumu yaliyoungwa mkono na Rais Magufuli ni ishirini na moja
kama ifuatavyo
1. Serikali, kupitia Msajili wa Makampuni ichukue hatua za kisheria dhidi ya
kampuni ya Acacia Mining Plc ambayo imekuwa inaendesha shughuli zake nchini
kinyume na matakwa ya Sheria.

2. Serikali idai kodi na mrahaba kutoka kwa makampuni yote ya madini ambayo
yamekwepa kulipa kodi na mrahaba stahiki kwa mujibu wa sheria.3. Serikali iendelee kuzuia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi mpaka hapo
makampuni ya madini yanayodaiwa yatakapolipa kodi, mrahaba na tozo stahiki kwa
mujibu wa sheria.

4. Serikali ianzishe utaratibu utakowezesha ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji
wa makinikia (smelter) ili kuondoa upotevu wa mapato na kutengeneza ajira kwa
watanzania.5. Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya
waliokuwa Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali na Manaibu wao, Wakurugenzi wa
idara za mikataba, na Makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya Nishati na
Madini na watumishi wengine wa Serikali na watu wote waliohusika katika kuingia
mikataba ya uchimbaji madini, utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini na
kuongeza muda wa leseni, watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini,
makampuni yaliyohusika kuandaa nyaraka za usafirishaji wa makinikia(Freight
Forwarders(T)Ltd na makampuni ya upimaji wa madini kwa kuvunja sheria za nchina
upotoshaji.6. Serikali ifute utaratibu wa kupokea malipo ya mrahaba ya asilimia 90 na
kusubiri malipo ya asilimia 10 kulipwa baadaye wakati makampuni hayo ya madini
huyauza madini hayo na kupewa fedha taslimu kwa mkupuo.7. Serikali ifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa Watumishi wa idara ya
walipakodi wakubwa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kushughulikia madai
ya kodi ambayo Mabaraza ya Rufaani ya Kodi na Mahakama zimekwisha yatolea
uamuzi na vilevile ichunguze mienendo ya watumishi wa mabaraza ya Kodi kwa
kutotolea maamuzi ya kesi za kodi kwa muda mrefu kuhusu mashauri yaliyochukua
muda mrefu kukamilika katika vyombo hivyo.8. Benki Kuu ya Tanzania ifuatilie malipo ya fedha za kigeni yanayotokana na
mrahaba kwa mauzo ya madini.9. Serikali ianzishe utaratibu wa kulinda maeneo ya migodi na viwanja ndege
vilivyopo vigodini ili kudhibiti vitendo vya hujuma vinavyoweza kuwa vinafanywa
na makampuni ya migodi ikiwemo utoroshaji wa madini.10. Sheria iongeze kiwango cha adhabu zilizoainishwa kwa makosa ya ukiukwaji
wa Sheria ya Madini na Sheria za Kodi.11. Serikali kupitia wataalum wabobezi katika majadiliano na mikataba
(expert in negotiation and contract) wapitie mikataba yote mikubwa ya uchimbaji
madini ipitiwe (review) na kufanya majadiliano na makampuni ya madini ili
kuondoa misamaha yote ya kodi isiyokuwa na tija kwa taifa na badala yake kuweka
masharti yenye tija kwa pande zote mbili kwa kuzingatia maslahi ya nchi;12. Sheria iweke kiwango maalum cha asilimia ya hisa ambazo zitamilikiwa na
Serikali katika makampuni yote ya madini nchini. Aidha, Sheria ielekeze
Serikali kufanya majadilaino ili kuwezesha Serikali kununua hisa katika
makampuni ya uchimbaji madini ili kuiwezesha kupata mapato zaidi na ushiriki
katika maamuzi muhimu katika biashara ya madini.13. Serikali iunde chombo cha kusimamia biashara ya usafirishajibidhaa nje
ya nchi kupitia bandari kama ilivyokuwa kama lilivyokuwa shirika la NASACO ili
kudhibiti biashara haramu na kuondoa mianya ya ukwepaji kodi.14. Sheria itamke bayana kuwa madini ni mali asili ya watanzania na iwekwe
chini ya udhamini na uangalizi wa Rais kwa manufaa ya watanzania.15. Sheria itamke bayana kuwa mikataba yoyote ya uchimbaji mkubwa wa madini
(Mining Development Agreement) isiwe ya siri na lazima yaridhiwe na Bunge kabla
ya kuanza kutekelezwa.16. Sheria itoe masharti ya wazi ya kuzingatiwana iondoe uhuru wa mamlaka ya
(discretionary powers) za Waziri wa Nishati na Madini, kamishna wa madini na
maafisa madini wakanda katika utoaji wa leseni za uchimbaji madini.17. Sheria ya madini iweka masharti kwamba mwombaji wa leseni ya uchimbaji
mkubwa wa madini lazima yaoneshe mchanganuo wa kina kuhusu namna mafunzo
kwawazawa yatakavyotolewa kwa lengo la ajiri kama wataalam na kuchukua nafasi
za uendeshaji wa migodi husika na kupunguza au kuondoa kabisa wataalam kutoka
nje ya nchi.18. Sheria ielekeze makampuni ya madini kuweka fedha zinazotokana na mauzo
ya madini katika benki zilizopo nchini ili kuimarisha uchumi wa nchi na kuondoa
mianya ya ukwepaji wa kodi na tozo mbalimbali.19. Serikali ipitie na kufanya marekebisho au kufuta na kubadili kabisa
Sheria ya Madini na Sheria za Kodi ili kuondoapamoja mambo mengine masharti
yote yasikuwa na manufaa kwa taifa ikiwa ni pamoja na masharti yaliyomo kwenye
kifungu thabiti (stability provision).20. Serikali igharimie nakutoa mafunzo kwa watumishi wa Serikali ili
kuwapatia uelewa na weledi katika nyanja ya majadiliano na uendeshaji wa
mashauri yatokanayo na mikataba ikiwemo ya mikataba ya madini (skills in
negotiation and arbitration).21. Serikali kupitia Kamishna wa Madini iwe inafanya ukaguzi wa mara kwa
mara kaw makampuni ya madini ili kujihakikishia uzingatia au ukiukwaji wa
Sheria na taratibu za uendeshaji na kuchukua hatua ipasavyo.


IMETOLEWA NA:

KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO


Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP