Polisi nchini Uingereza imewataja wanaume wawili kati ya watatu waliofanya shambulio katika London Bridge siku ya Jumamosi na kuwauwa watu saba kabla ya kuuawa kwa risasi .

Mmoja wao alikuwa Khuram Butt, alikuwa akitambuliwa na huduma za usalama za Uingereza.
Aliwahi kuonekana kwenye kipindi cha Televisheni mwaka jana kilichoangazia kundi lenye itikadi kali linalounga mkono Islamic state .
Wote waliokuwa wamekamatwa na polisi kufuatia mauaji hayo wameachiliwa bila mashtaka
Vigil in Potters Field ParkHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionIbada ilifanyika eneo la Potters Field Park karibu na London Bridge