Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 11, 2017

RATIBA YA MAZISHI YA NDUGU YETU BIKIRA WA KISUKUMA KESHO

Meneja Mkuu wa Radio Efm na TV-E,  Dennis Ssebo, ametoa ratiba ya mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wao Seth Katende ‘Bikira wa Kisukuma‘, amesema kesho saa tatu asubuhi mwili wa marehemu utachukuliwa kutoka nyumbani kwa baba yake Changanyikeni, jijini Dar es Salaam, kuelekea viwanja vya Leaders Clubambako utapokelewa na wazazi wake, viongozi wa serikalina wadau mbalimbali.

Aliyekuwa mtangazaji EFM. Marehemu, Seth Katende ‘Bikira wa Kisukuma’.
Baada ya hapo patafanyika misa ya kumuombea marehemu na kufuatiwa na salamu za rambirambi ambapo kuanzia saa 6 hadi saa 8 utakuwa ni muda wa kumuaga marehemu ambapo safari ya kuelekea makaburini kwa ajili ya mazishi itaanza.
Mazishi yatafanyika kuanzisha saa 9 alasiri katika makaburi ya Kinondoni, ambapo wananchi wa Dar es Salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi kumzika ndugu yao Seth Katende.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa; jina lake lihimidiwe!
Ratiba ya mazishi.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP