Mchezaji wa tenisi anayeorodheshwa nambari miongoni mwa wanawake Serena Williams amepiga picha za utupu katika kurasa ya kwanza ya jarida la August Vanity Fair.
Nyota huyo wa tenisi alibaini kwamba alikuwa akitarajia mwanawe wa kwanza na mpenziwe Alexis Ohanian kabla ya michezo ya Australia Open mnamo mwezi Januari.

Aliambia jarida hilo kwamba hakutarajia chochote hadi alipobaini kwamba alikuwa mgonjwa wakati wa mazoezi.
Picha ya utupu ya Serena katika jarida la vanity fairHaki miliki ya pichaVANITY FAIR
Image captionPicha ya utupu ya Serena katika jarida la vanity fair
Lakini rafikiye alishuku kwamba huenda ni mjamzito na kuamua kuchukua vipimo.
Serena alifanya vipimo hivyo wakati alipokuwa akipigwa picha na kampuni moja ndani ya Hoteli moja nchini Australia na kusema kuwa alipigwa na butwaa wakati alipopata majibu.
Serena Wiliams na mpenzi wake Alexis OhanianHaki miliki ya pichaAFP
Image captionSerena Wiliams na mpenzi wake Alexis Ohanian
''Mungu wangu, hii haiwezekani- ni lazima nicheze mchuano mmoja'',alisema. Nitacheza vipi mashindano ya Australian. Nilikuwa nimepanga kushinda taji la Wimbledon mwaka huu''.
Rafikiye Jessica baadaye alitumwa kununua vifaa vyengine vitano vya kupima uja uzito ili kumthibitishia Serena kwamba ni mjamzito.
Vipimo vyote vilithibitisha.Habari hiyo pia ilisema vile Serena na mpenziwe walivyokutana 2015.
Serena Williams
Image captionSerena Williams
Alimchumbia Disemba katika meza hiyo hiyo ya Cavalieri katika hoteli moja huko Italy ambapo walikutana.