Walinzi wa mbuga nchini Afrika Kusini wanawattafuta simba wanne waliotoroka kutoka mbuga ya kitaifa.
Simba hao walitoroka kutoka mbuga ya Kruger siku ya Jumapili na mara ya mwisho walionekana katika kijiji cha Matsulu.
Usimamizi wa mbuga hiyo sasa umewataka wenyeji kuchukua tahadhari.
Haijabainika vile simba hao walifanikiwa kutoroka kutoka mbuga hiyo inayozungukwa na ua.
Mbuga ya kitaifa ya Kruger ni moja ya mbuga kubwa zaidi barani Afrika ikiwa na ukubwa wa kilomita 19.485 mraba.
Kisa hiki kinatokea baada ya simba wengine watano kutoroka mbuga hiyo mwezi Mei. Wanne walipatikana lakini mmoja bado hajulikani aliko.
0 Comments