Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jul 3, 2017

TANZANIA YAIFUNGA AFRIKA YA KUSINI NYUMBANI KWAO 1-0

Elius Maguri akishangilia goli moja  lililoizamisha timu ya Afrika ya Kusini dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania katika  michuano ya kombe la Cosafa hapo jana. 

Bao la dakika ya 17 la mshambuliaji Elias Maguri lilitosha kuipeleka Stars katika nusu fainali ya michuano katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Royal Bafokeng, Rusternburg.
Tanzania sasa itamenyana na Zambia siku ya Jumatano katika mchezo wa nusu fainali, wakati Afrika Kusini wanaangukia kwenye michuano ya Plate, inayoshirikisha timu zilizotolewa hatua ya robo fainali.
Katika mchezo wa pili wa michuano hiyo Zimbabwe waliwachapa Swaziland kwa mabao 2-1.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP