Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
SERIKALI inatoa sh. bilioni 18.77 kwa ajili ya kugharamia elimu bure ili kila mtanzania apate elimu bora na faida yake kwa serikali hiyo ni kuona wanafunzi wanafaulu darasa la Saba na Kidato cha Nne na kuendelea na elimu ya kidato cha tano na hadi chuo kikuu.
Hayo ameyasema leo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati wa uzinduzi mabweni katika shule ya sekondari Nasibugani ambayo ujenzi wake uko katika hatua ya mwisho pamoja na Shule ya Sekondari Mwinyi ambayo ujenzi umekamilika kwa kuingia wanafunzi katika mabweni hayo wilayani Mkuranga mkoani Pwani .
Profesa Ndalichako amesema serikali ya awamu ya tano imeondoa imeondoa gharama katika shule ya msingi na sekondari ili kuondosha mzigo kwa wazazi wengine ambao walikuwa wanashindwa kugharamia elimu hiyo.
Amesema mabweni katika shule ya sekondari Nasibugani na Mwinyi zenye Kidato cha Kwanza hadi Sita ni kuongeza sehemu ya kumwezesha mwanafunzi kusoma kwa muda mrefu na kuweza kondokana na vishawishi vinavyopatikana mtaani.
Aidha amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha shule mbalimbali ikiwemo pamoja na makazi ya walimu yaliyo bora pamoja na huduma zingine ikwemo umeme katika shule ya Sekondari Nasibugani.
Amesema kuwa Mkuranga iko nyuma kielimu ni ukweli usiofichika hivyo walimu pamoja na watendaji kuhimiza suala la elimu ili viwanda vilivyopo na wanamkuranga wanufaike na sekta hiyo.
Waziri Profesa Ndalichako amempongeza Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega kuanzisha Program kwa wanafunzi wa sekondari kuwa Hakuna Kufeli.
Amesema Program hiyo ifanywe kwa vitendo kwa wanafunzi kujitoa zaidi kusoma kwani mtihani uko karibu lakini wakitumia program hiyo watafanya vizuri na kuondoa sifuri katika shule zao na kuanza daraja la kwanza hadi la tatu.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amesema kuwa wanaomba chuo cha Ufundi katika wilaya hiyo ili vijana waweze kujiunga na kuweza kutumika katika sekta ya viwanda vilivyojengwa Mkuranga.
Amesema kuwa zaidi ya vijana 900 hawana ajira hivyo chuo cha ufundi ni sehemu sahihi kwa vijana na wataendelea kuongeza mwaka hadi mwaka kadiri wnavyohitimu.
Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega amesema kuwa jitihada mbalimbali katika kuboresha miundombinu ya shule pamoja na serikali kuongeza walimu.Amesema kuwa wanafunzi wanavyofanya vizuri ni furaha na kuweza kuwa nguvu ya uandaji wa vijana katika mapinduzi ya elimu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akizindua mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Nasibugani iliyopo Wilaya ya Mkuranga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akipanda mti katika shule ya Sekondari Nasibugani.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akizindua mabweni mawili yaliyokamilika katika shule sekondari Mwinyi iliyopo Wilaya ya Mkuranga.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza wananchi na wanafunzi katika shule ya Sekondari Nasibugani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza wananchi na wanafunzi katika shule ya Sekondari Nasibugani.
Sehemu ya mabweni na nyumba za walimu ambazo zimefikia hatua ya boma
Sehemu ya mabweni na nyumba za walimu ambazo zimefikia hatua ya boma
0 Comments