Fundi akichomelea vyuma kwa ajili ya kufunga nyavu ikiwa ni marekebisho ya mwisho katika uwanja wa shule ya Sekondari Ikungi, wilaya ya Ikungi mkoani Singida kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya ligi ya mpira wa miguu ya Ikundi Elimu Cup 2017 wilayani Ikungi.
Kauli mbiu katika mashindano hayo ni " Changia, Boresha Elimu Ikungi.
Na George Binagi, BMG
Mashindano hayo yatashirikisha timu mbalimbali kutoka Kata 28 wilayani Ikungi yakilenga kuhamasisha wananchi na wadau wengine wa elimu kushiriki katika kutatua changamoto za elimu ikiwemo uhaba wa madarasa, nyumba za waalimu, maabara pamoja na vyoo vya shule.
Hii ni baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu kuteuliwa kuwa mlezi wa mfuko wa elimu wilayani humo na hivyo kuamua kuanzisha michuano hiyo ili kuleta chachu kwa wananchi na wadau mbalimbali kuchangia masuala ya kielimu.
Jumamosi timu ya soka ya Ikungi United na inakuwa ikimenyana na timu ya Puma ambapo mchezo huo utatanguliwa na mchezo kati ya madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Singida dhidi ya madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Katika mchezo huo wa awali timu ya madiwani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ikungi itaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu huku timu ya madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Singida ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe.Elias Tarimo.
Ufunguzi wa mashindano hayo utatanguliwa na shughuli ya ufyatuaji matofali ambapo kila Kata wilayani Ikungi imetakiwa kufyatua matofali yasiyopungua 10,000 ili kusaidia ujenzi wa madarasa, nyumba za waalimu na vyoo vya shule.
Mwl.Seth Raban Mwakalasya ambaye ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya ligi ya ligi ya soka ya Ikungi Elimu Cup 2017 yanayotarajiwa kuanza katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jumamosi Agosti 19 katika uwanja wa shule ya sekondari Ikungi.
Timu ya soka ya Ikungi United Sports Club ikifanya mazoezi katika uwanja wa shule ya msingi Ikungi jioni ya leo
Ikungi United Sports Club wakifanya mazoezi katika uwanja wa shule ya msingi Ikungi jioni ya leo
Ikungi United Sports Club watamenyana na timu ya Puma katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Ikungi Elimu Cup 2017
Timu ya Ikungi United Sports Club ikiwa kwenye mazoezi hii leo jioni
Nahodha wa timu ya Ikungi United Sports Club, Lazaro John Francis (pichani) amesema maandalizi yao yako vizuri na kwamba michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017 itakuwa na ushindani mkubwa hivyo wapenzi wa soka wategemee soka la kuvutia kwenye michuano hiyo
Kocha wa timu ya soka ya Ikungi United Sports Club, Danny Ayoub amesema kikosi chake kimejipanga vyema na kwamba michuano itaweza kuiwezesha timu yake kusonga mbele kimichezo nchini ikifuata nyayo za kaka zao Singida United.
Kikosi cha Ikungi United Sports Club kikiwa kwenye tathmini fupi baada ya mazoezi ya hii leo jioni
Kocha wa kikosi cha Ikungi United Sports Club akitoa tathmini fupi baada ya mazoezi ya timu hiyo jioni ya leo ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kwenye michuano ya Ikungi Elimu Cup 2017 katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambapo michuano hiyo itafunguliwa jumamosi Agosti 19,2017 huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi.
Kauli mbiu katika mashindano hayo ni " Changia, Boresha Elimu Ikungi.
0 Comments