Saudi Arabia imekuwa mwenyeji wa mazungumzo na wajumbe waandamizi kutoka familia ya kifalme ya Qatar kwa mara ya kwanza tangu serikali ya Saudi Arabia na washirika kukata uhusiano na Qatar miezi miwili iliyopita.
Mfalme wa Saudi Arabia ameamuru mpaka kati ya nchi hizo mbili ufunguliwe ili kuruhusu raia wa Qatar kushiriki katika ibada ya kila mwaka ya hijja mwishoni mwa mwezi huu.
Pia amejitolea kulipia gharama za ndege kwa wale watakaoshiriki ibada hiyo.
Qatar imetengwa kiuchumi na kidiplomasia na Saudi Arabia, Egypt, Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE baada ya kuituhumu kuunga mkono makundi ya wapiganaji wa kiislamu, tuhuma ambazo imekuwa ikizikana.
|
0 Comments