Maafisa nchini Libya wamesema Hashem Abedi, kaka wa mshambuliaji wa bomu la kujitoa mhanga, lililouwa watu 22 katika mji wa Manchester, Uingereza atafikishwa mahakamani mjini Tripoli kwa kuhusika na shambulio hilo.

Hashem Abeid aliyekuwa na miaka 20 alikamatwa mjini Tripoli muda mfupi baada ya mlipuko huo wa Manchester.
Mkurugenzi wa upelelezi katika kesi hiyo nchini Libya, Sadiq Al Sour ameiambia BBC kwamba dalili zote zinaonesha mshtakiwa huyo ndiye aliyemsaidia mdogo wake Salman.
Baba yao ambaye pia alikamatwa, ameachiwa kutoka rumande.