Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan ametoa wito kwa Bodi na Menejimenti ya NBC na Mabenki mengine
kuwa kuanzia sasa Taasisi zote za fedha ziweke kipaumbele cha kwanza
katika kuwezesha kuendeleza viwanda nchini hasa viwanda vidogo vidogo na
vya kati vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu
na madini ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.Pia viwanda ambavyo
vinatumia teknolojia ya kati na nguvu kazi zaidi ( labour intensive
technology).




Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akihutubua kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya NBC.



Mhe. Samia alisema mabenki mengi yameendelea kutoza riba ubwa hivyo
kupelekea wananchi wa kipato cha chini hivyo aliwataka Wataalamu wa NBC
na Sekta za Fedha kwa ujumla kutafuta suluhisho la riba zisizo rafiki
kwa walio wengi ili amana pamoja na mikopo iweze kuongezeka.



Makamu wa Rais aliziagiza Bodi na Menejimeni ya NBC na Mabenki yote
nchini kuzingatia Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha, alisema "
Serikali ya Tanzania haitomuonea mtu haya na itachukua hatua kali dhidi
ya benki au Taasisi yeyote itakayobainika kukiuka matakwa ya sheria
hiyo."



Mwisho Makamu wa Rais aliipongeza benki ya NBC kwa kuweza kutoa gawio la
Shilingi Bikioni 1.2 mwaka huu 2017 kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa
kwake.