Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa
Makame Mnyaa Mbarawa(katikati), akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu
(CEO), wa Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Tanzania, Bw. Le
Van Dai (kulia) wakati wakisaini mkataba wa kusambaza mawasiliano ya simu kwa


kujenga miundombinu maeneo ya vijijini, chini ya Mradi wa sita wa kufikisha
mawasiliano kwa wote, kwenye makao makuu ya UCSAF barabara ya
Bagamoyo, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Agosti 18, 2017. UCSAF
imesaini makubaliano kama
hayo na makampuni mengine ya simu hapa nchini ikiwemo, Vodacom Tanzania PLC,
Airtel, tigo na TTCL.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Mawasiliano Kwa Wote Nchini,
(UCSAF), umesaini mkataba na makampuni matano ya simu hapa nchini wa
utekelezaji wa Mradi wa Sita wa Kupeleka mawasiliano ya simu kwa
wote.
Mikataba hiyo imesainiwa mbele ya
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Manyaa
Mbarawa.
  Makampuni yaliyotia saini
mkataba huo ambao utayawezesha, kujenga miundombinu ya kupeperusha
mawasiliano ya simu kwenye mmbalimbali hususan vijijini ni pamoja na
Halotel, Airtel, Vodacom Tanzania PLC, TTCL na TIGO.
Waziri Profesa Mbarawa alishuhudia
Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF kwa niaba ya Mfuko, akisaini mikataba
hiyo na Maafisa Watendaji Wakuu wa makampuni hayo mbele ya waandishi
wa habari.




Kwa
mujibu wa maafisa wa UCASAF, kusainiwa kwa mikataba hiyo ni moja ya kutekekeleza
malengo makuu ya Mfuko ambayo ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya
mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano
hafifu.
Lakini
pia ni kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa
huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini yenye mawasiliano
hafifu.
Malengo mengine ni pamoja na
Kuhamasisha maendeleo ya
kijamii na kiuchumi katika maeneo
ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu;
Kutengeneza
mfumo kwa ajili ya upatikanaji wa mitandao ya mawasiliano na huduma rahisi na
zenye ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji katika soko la
kiushindani;
Maafisa
hao wamesema lengo linguine ni kuhamasisha utoaji wa huduma bora katika viwango
nafuu na kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasilianpo inapatikana
vijijini na sehemu za mijini zenye mawasiliano hafifu kwa bei
nafuu.
Kwa
upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa, amewahakikishia wawekezaji ushirikiano uklio dhahiri kutoka serikalini
na kuwataka, waongeze kasi ya uboreshaji wa mawasliano ya simu ili wananchi
hususan wa vijijiniwaweze kutumia teknolojia ya mawasiliano kuharakisha
maendeleo yao.




 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa, akitoa hotuba yake
Mwenyekiti
wa Bodi ya UCSAF, Bw. Joseph Kilongola, akizungumza kwabla ya
kumkaribisha Profesa Mbarawa kutoa hotuba
 Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, akielezea
lengo la kusainiwa kwa mikataba hiyo ya utekelezaji wa Mradiwa sita wa
kupeleka mawasiliano kwa wote.
 Baadhi ya wawakilishi wa
makampuni ya simu
 Bi. Beatrice Singano Malya
kutoka Airtel, akifurahia hotuba.
 Baadhi ya maafisa wa makampuni
ya simu na UCSAF
 Afisa kutoka kampuni ya
Halotel
Afisa
Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter
Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice
Suingano Malya, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa sita wa
kepeleka mawasiliano ya simu kwa wote.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa,
(kulia), akimpongeza Mwakilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi.
Beatrice Singano Malya, mara baada ya Airtel kusaini mkataba wa sita wa
Mradi wa kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote na Mfuko wa Mawasiliano
kwa Wote, (UCAF), jijini Dar es Salaam, Agosti 18,
2017

Afisa
Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter
Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice
Singano Malya wakisaini mkataba wa Mradi wa sita wa kupeleka mawasiliano kwa
wote.