Mtoto
aliyeungua na kushindwa kuendelea na masomo mkoani Mtwara ametibiwa 
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na sasa anaweza kuendelea na 
masomo pamoja na kufanya shughuli zake za kawaida.

Mtoto
huyo aliungua moto baada ya kusukumwa na mwenzake shuleni na hivyo 
kuungua mikono yote miwili na kusababisha vidole kujikunja na 
kushikamana.Baada ya kufikishwa Muhimbili madaktari bingwa walifanyia 
upasuaji na sasa amepona.

Daktari
Bingwa wa Upasuaji, Ibrahimu Mkoma amesema mtoto Mwanahidi Hamisi 
aliungua miaka saba iliyopita na mikono yake kuadhirika na kushindwa 
kufanya kazi yoyote.

Amesema
mwaka 2015 mtoto huyo alifanyiwa upasuaji mkono wake wa kulia katika 
Hospitali ya CCBRT na kwamba sasa anaendelea vizuri.Dk Mkoma amesema 
Juni 7, 2017 Muhimbili ilimpokea mtoto huyo na baada ya kufanyia 
uchunguzi walimfanyia upasuaji mkono wa kushoto na kunyoosha viungo 
katika vidole vyake ambavyo vilikuwa vimejikunja.




“Baada
ya kuungua moto vidole vyake vilishikana na viungo kujikunja, lakini 
tumefanikiwa kuvinyoosha viungo hivyo na sasa Mwanahidi anaendelea 
vizuri na matibabu,” amesema Dk Mkoma.Amesema mtoto huyo sasa anaweza 
kufanya kazi mbalimbali kama kufua na kwamba anaweza kundelea na shule 
tofauti na awali baada ya kuungua.

Mama
wa mtoto huyo, Amina Mohamed Mkadengile ameambiwa kwamba anapaswa 
kumfanyia mazoezi mtoto wake ili aimarike zaidi.“Daktari amenielekeza 
jinsi ya kumfanyia mtoto mazoezi, nitakuwa nafanyia mazoezi katika 
Hospitali ya Mkoa ya Ligula mkoani Mtwara. Nawashukuru sana.