Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameambia umati wakati wa sherehe za siku ya mashujaa kwenye mji mkuu wa Harare, kuwa watu ambao waliwaua wakulima wazungu wakati wa mabadiliko ya mifumo ya ardhi nchini humo hawatashtakiwa.

"Ndio tuna wale waliouwawa wakati walipinga. Hatuwezi kuwashtaki wale waliowaua. Ninauliza mbona tunawashtaki?" alisema Mugabe.
Wakati wa ukoloni, ardhi nzuri ilitengewa wazungu na mwaka 2000, bwana Mugabe aliongoza kutwaliwa kwa ardhi hiyo kutoka kwa wakulima 4000.Rais Mugabe awali alikiri kuwa mifumo ya ardhi ya nchi hiyo ilifeli na mwaka 2015 alisema:
"Nafikiri mashamba tuliyowapa watu ni makubwa, hawawezi kuyasimami.
Kutaliwa ghafla mashamba kutoka kwa wakulima wazungu, inaonekana kuwa sababu kuu ya kuporomoka kwa uchumi wa Zimbabwe tangu mwaka 2000.