Rais wa Marekani Donald Trump ameanza ziara ya kuizuru Texas wakati taifa lake likiendelea kukabiliana na dhoruba kali ambayo imevunja rekodi kwa kiwango kikubwa cha mvua katika siku chache zilizopita.

Katika eneo la Corpus Christi mahali ambako awali kulishuhudiwa dhoruba hiyo, aliwashukuru wafanyazi wa vitengo vya dharula ambao walikuwa wakikabiliana na mafuriko ambapo alielezwa mafanikio makubwa ya uokozi.
Naye gavana , Greg Abbott, amemtaka rais huyo kutambua changamoto kubwa zinazoukabili mji wa Texas. Huko mjini Houston, Mabwawa mawili yameanza kufurika , kumeshuhudiwa Kuongezeka kwa mafuriko makubwa .
Pia Meya Sylvester Turner amesema kwamba mji wake umeomba msaada wa dharula wa shirikisho la nyumba kwa watu wengine elfu kumi kupatiwa makazi ya dharura.