Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Ndg Salum A. Kalli akitoa salamu za CCM wakati wa uzinduzi wa Ugawaji wa
vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam.

Zoezi la Uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam


Na Mathias Canal, Dar
es salaam

Chama Cha Mapinduzi
Wilaya ya Ubungo kimetoa heko kwa viongozi wa serikali Wilaya ya Ubungo chini
ya Mkuu wa Wilaya Mhe Kisare Makori kwa ushirikiano wake katika utendaji na
kuipaisha Wilaya katika tathmini za mafanikio kwa wananchi wake ukilinganisha
na ugeni wa Wilaya kwani ilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2016.

Sambamba na Mkuu huyo
wa Wilaya kwa ushirikiano mkubwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John
Lipesi Kayombo sawia na watumishi wote wameifanya Manispaa ya Ubungo kuwa
kwenye rekodi ya Manispaa zinazothamini wananchi wake hususani wazee.

Pongezi hizo zimetolewa
na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Ndg Salum Kalli wakati wa
uzinduzi wa Ugawaji wa vitambulisho vya awali 7296 vya matibabu Bure kwa Wazee
katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam dhifa
iliyofanyika katika viwanja vya TP Sinza E.

Kalli
alitoa salamu za Chama hicho mbele ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy A. Mwalimu ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi huo ambaye pia Mhe Ummy
aliahidi kutoa Bima za afya kwa watoto 100 wenye umri chini
ya miaka 18 waishio katika mazingira magumu sambamba na kujenga wodi ya wazazi,
watoto na maabara ya damu kwenye kituo kimoja cha afya.

Alisema kuwa uzinduzi
huo wa ugawaji wa vitambulisho ni kuonesha umma wa watanzania kuwa Wilaya ya
Ubungo inawajali Wazee ikiwa ni Sehemu ya utekelezaji wa ilani ya ushindi ya
Chama Cha Mapinduzi katika kipindi Cha mwaka 2015-2020.

Alisema
kuwa katika Sura ya nne, ibara ya 50 (P) inaeleza kuwa Halmashauri
zitahakikisha wazee wanatambuliwa na kupewa matibabu bure katika Hospitali za
serikali hivyo Manispaa ya Ubungo imetekeleza mkataba wa CCM na wananchi kwa
vitendo ndani ya miaka miwili kabla ya kumalizika miaka mitano ya ahadi.

Kalli
alisema kuwa pamoja na jambo hilo pia Wilaya ya Ubungo inapaswa kusimama kidete
katika shughuli zingine mbalimbali ili kuwaletea maendeleo wananchi kutokana na
imani kubwa walioionyesha Octoba 25, 2015 kwa kutoa ridhaa kwa Chama Cha
Mapinduzi.

Kalli
aliahidi mbele ya wahudhuriaji wa dhifa hiyo kuwa CCM itaendelea kuwaletea
maendeleo wananchi huku akimpongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe
Boniface Jackobo kwa kuiishi na kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo.

“Mgeni
rasmi naahidi mbele ya hadhara hii kuwa CCM tutaendelea kuja mara kwa mara
katika ofisi za serikali kukagua utekelezaji wa ilani ya ushindi mahali
tutakapobaini kuwa ilani haitekelezwi tutakemea vikali kwa maslahi ya wananchi
na Taifa kwa ujumla wake”




Wilaya
ya Ubungo imekuwa Walaya ya pili katika Jiji la Dar es salaam kutekeleza agizo
la serikali lililotolewa na Waziri Mkuu kwenye maadhimisho ya siku ya Wazee
Octoba 1, 2009 kuwa Hospitali zote na Vituo vya Afya vya Umma kutenga dirisha
na watumishi maalumu wa Afya kwa ajili ya kutoa Huduma za matibabu bure kwa
Wazee.

MWISHO