Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, FortunatusMuslim akizungumza na waandishi habari hawapo pichani juu hatua ambazo wanazichukua kwa madereva wanakiuka sheria za usalama barabarani, leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  MADEREVA saba (7) wa Mabasi yaendayo  mkoani wamefutiwa leseni zao pamoja na kufutiwa madaraja ya leseni hizo kutokana na kukiuka sheria za usalama barabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, FortUnatus Muslim amesesema kuwa madereva saba hao wamekiuka sheria za usalama na kwa mamlaka yake amefuta leseni zao kwa kipindi cha miezi sita na wanatakiwa kurudi darasani kwa kipindi cha miezi hiyo na kuhakikiwa upya kupewa leseni hizo.
Amesema kuwa madereva hao walikuwa wakiendesha mabasi kilomita 90 kwa saa ambapo kikosi cha usalama barabarani kiliweka  mahabusu  na kulipa faini kati ya sh. 100,000 hadi sh. 300,000 na kupoteza sifa za kuwa madereva.
Muslim amasema kwa mamlaka aliyopewa kwa anafuta leseni hizo kwa madaraja ya C na E kwa madereva ili warudi kusoma juu ya jinsi ya kujihami wanavyoendesha vyombo vya moto vva abiria na mizigo kibiashara kwa miezi sita hiyo.
Madereva hao Hamad Salum,  Kija Mayenga, Isack Mbijina, Hassan Semazua, Stanley Mosha, Abdallah Hussein yuko mahabusu kwa kokosa kulipa faini pamoja na Sempunda Yusufu.

Aidha madereva watatu wamefungiwa leseni zao za kubeba abiria kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kusababisha ajali.

Madereva hao Ismail Nyami alisababisha ajali iliyoua watu wawili na kujeruhi 42 iliyotokea Septemba 23 mkoani Ruvuma mkoani Ruvuma ,, Mseka Salum alisababisha ajali iliyoua  Mtu mmoja  na kujeruhi 25 Kishapu mkoani Shinyanga, Malick Hassan alisababisha ajali kwa kugonga Ng’ombe  na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi Sita.

Muslim amesema kuwa operesheni zitaendelea kuendesha hadi majira ya usiku hivyo madereva wazingatie sheria za usalama barabarani.