Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama amesema kuwa hakuweza kuzuia machozi yake alipomfikisha mwanawe mkubwa Malia katika chuo kikuu.
Ilikuwa kama ''upasuaiji uliofanyika hadharani'', rais huyo wa zamani alizungumzia kuhusu wakati alipomfikisha Malia katika chuo kikuu cha Harvard.
''Nilifurahi kwamba sikububujikwa na machozi mbele yake'', alisema bwana Obama.
''Lakini nilipokuwa nikirudi, maafisa wa jinai hawakuwepo nikaangalia mbele nikijifanya kwamba hawanisikii nikinungunika na kufuta pua yangu.Ilikuwa vigumu''.
Bwana Obama alielezea wakati huo siku ya Jumatatu wakati wa hafla ya wakfu wa Beau Biden. Shirika hilo la kusaidia jamii lilianzisha kwa heshima ya mwana{marehemu} wa aliyekuwa makamu wa rais Joe Biden
''Mwisho wa maisha yetu chochote kile ambacho utakuwa umefanikiwa, ambayo tutayakumbuka ni maisha mazuri ya wana wetu na baadaye kile kitakacholetwa na wajukuu zetu'', alisema Obama.
|
0 Comments