Karibu tani nne za cocaine za thamaniya karibu dola milioni 260 imekamatwa na maafisa wa kimataifa katika pwani ya Hispania.
Madawa hayo ya kulevya yalipatikana kwenye mashua moja kati ya Madeira na visiwa vya Azores.
Haijulikani ni wapi madawa hayo yalikuwa yakipelekwa. Wahudumu wa mashua hiyo kutoka Uturuki na Azerbaijan walikamatwa.
Chombo hicho kilichikuwa na bendera ya Comoros kulipelekwa bandari ya Hispania ya Cadiz.
Haki miliki ya pichaEPAImage captionKaribu tani 4 za cocaine zakamatwa HispaniaHaki miliki ya pichaEPAImage captionKaribu tani 4 za cocaine zakamatwa Hispania
Oparesheni hiyo ya pamoja ileondeshwa na maafisa wa forodha wa Hispania na polisi.
Kumekuwa na visa vingine viwili vya kukamatwa kwa madawa ya kulevya miezi ya hivi karibuni.
Raia 13 wa Hispania na mmoja raia wa Morocco walikamatwa siku ya Jumatatu kufuatia kile kilichoaminika kuwa kukamatwa kiwango kikubwa cha coccaine kwenye taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.
Haki miliki ya pichaEPAImage captionKaribu tani 4 za cocaine zakamatwa HispaniaImage captionKaribu tani 4 za cocaine zakamatwa Hispania
0 Comments