Leicester City wamemfuta kazi kocha wao Craig Shakespeare miezi minne tu baada ya kusaini kandarasi ya miaka minne ili kuchukua kazi hiyo kwa mkataba wa kudumu.
The Foxes kama wanavyojiita wako nafasi ya tatu kutoka chini katika jedwali la ligi ya Uingereza na hawajashinda mechi yoyote miongoni mwa mechi sita walizocheza.
Shakesspeare mwenye umri wa miaka 5, alimrithi Claudio Ranieri mnamo mwezi Februari kwa muda.
Baada ya kuiongoza Leicester na kuweza kumaliza katika nafasi ya 12 alipewa kazi ya kudumu mnamo mwezi Juni.
Shakespeare alishinda mechi 8 kati 16 akiwa mkufunzi wa timu hiyo msimu uliopita na kuisaidia klabu hiyo kufika katika robo fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Amefutwa kazi baada ya timu hiyo kupata sare ya 1-1 dhidi ya West Brom siku ya Jumatatau.
Mara ya mwisho kwa Leicester kucheza mechi sita bila ushindi Ranieri alifutwa kazi , miezi tisa baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda taji la ligi.
|
0 Comments