Rais wa eneo linalojisimamia nchini Uhispania la Catalonia ameshindwa kuthibitisha ikiwa ametangaza uhuru kwenye barua kwa serikali ya Madrid.
Uhispania ilikuwa imetoa muda hadi leo Jumatatu kwa Carles Puigdemont, kuthibitisha nia yake au eneo hilo litawaliwe moja kwa moja na Madrid.
Badala yake kiongozi huyo wa Catalonia alitaka kufanyika mazungumzo ndani ya miezi miwili inayokuja.
Bw. Puigdemont alitangaza uhuru wiki iliyopita baada ya kura ya maoni iliyokumbwa na utata laki mara moja akafuta kutanga rasmi eneo hilo kuwa huru ili kuruhusu mazungumzo.Sasa inafikiriwa kuwa Uhispania itaongeza muda wake hadi Alhamisi kwa Bw. Puigdemont kubadilisha msimamo wake kabla ya kujaribu kulitawala eneo hilo moja kwa moja.
Tarehe ya mwisho iliyotolewa kwa Carles Puigdemont ilikuwa na leo Jumatatu 08:00 GMT.
Baada ya kura ya maoni ya uhuru wiki mbili zilizopita ambayo ilitangazwa kuwa iliyo kinyume na sheria na mahakama ya katiba ya nchi hiyo, Bw Puigdemont alisaini tangazo la uhuru lakini akafuta kutekelezwa kwake.
Alisema alitaka mazungumzo na serikali ya Madris lakini hilo halijafanyika.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionUtawala wa Catalonia unasema zaidi ya watu 800 walijeruhiwa
0 Comments