Maafisa huko Catalalonia wanasema kuwa watu 337 wamejeruhiwa kwenye ghasia wakati polisi wanajaribu kuzuia kura ya maoni ya uhuru wa Catalonia
Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Zaidi ya 300 wajeruhiwa wakati wa kura ya uhuru Catalonia
Serikali ya Uhispania imeahidi kuzuia kura hiyo ambayo imetangazwa kuwa isiyo halali na mahakama ya katiba ya nchi hiyo.
Maafisa wa polisi wanawazuia watu kupiga kura huku wakichukua makaratasi ya kupigia kura na masanduku kutoka kwa vituo vya kupigia kura.
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Upigaji kura wa uhuru wa Catalonia waanza licha ya vizuizi vya polisi
Maafisa wa serikali ya Catalonia wametabiri idadi kubwa ya watu kujitokeza.
Makatasi ya kipigia kura yana swali moja tu: "Unataka Catalonia kuwa taifa huru na jamhuri?" Kuna masanduku mawili ya ndio na hapana.
Image caption Upigaji kura wa uhuru wa Catalonia waanza licha ya vizuizi vya polisi
Katika mji wa Girona polisi wa kuzima ghasia waliingi katika vituo vya kupigia kura kwa nguvu ambapo kiongozi wa eneo hilo alitarajiwa kupigia kura yake.
Picha za televisheni ziliwaonyesha wakivunja vioo vya kuingia kituo hicho na kuwaondoa kwa nguvu wale waliojaribu kupiga kura.
Haki miliki ya picha AFP/GETTY Image caption Upigaji kura wa uhuru wa Catalonia waanza licha ya vizuizi vya polisi
Hata hivyo shirika la habari la Reuters lilisema kuwa Bw Puigdemont alifanikiwa kupiga kura yake.
Wakati huo huo kwenye mji mkuu wa eneo hilo, Barcelona polisi walifyatua risasi za mipira kwa wale wanaounga mkono hatua ya kujitenga.
0 Comments