Waziri wa uchukuzi nchini Israel anataka kuchimbwa reli ya chini kwa chini kwenye mji wa zamani wa Jerusalem karibu na Ukuta wa Magharibi na kupewa jina la Donald Trump.
Yisrael Katz alisema kuwa anataka kumpa hushima rais huyo wa Marekani kufuatia uamuzi wake wa kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Ukuta wa Magharibi ndilo eneo takakatifu zaidi ambapo wayahudi wanaruhusiwa kuomba.
Reli hiyo mpya ya chini kwa chini na kituo cha treni na sehemu ya mradi wa reli ya mwendo kasi kutoka Tel Aviv ambayo inatarajiwa kuzinduliwa mwaka ujao.
Ujenzi wa awali eneo lililo karibu na Ukuta wa Magharibi ambalo hujulikana kwa waislamu kama Haram al-Sharif na kwa wayahudi kama Temple Mount imezua maandamano kutoka kwa wapalestina.
Map showing key holy sites in Jerusalem's Old City
Image captionMaeneo matakatifu katika mji wa zamani wa Jerusalem
Bw. Katz aliliambia gazeti moja la Israel la Yedioth Ahronoth kuwa kuongezwa kwa reli kutoka Tel Aviv kwenda Jurusalem ndio mradi muhimu zaidi kwa wizara ya uchukuzi.
Alisema kuwa ameidhinisha pendekezo kwa kamati ya reli ya Israel ya kujenga reli ya chini kwa chini ya umbali wa kilomita 3 kutoka Binyanei HaUma magharibi mwa Jerusalem kwenda Ukuta wa Magharibi iliyo eneo linalokaliwa na Jerusalem Mashariki.
Hali ya mji wa Jerusalem ndio chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina.
Israel inautaja mji wa Jerusalem kuwa mji wake mkuu huku wapalestina wakilitaja eneo la Jerusalem Mashariki lililotwaliwa na Israel wakati wa vita vya mwaka 1967 kama mji mkuu wa taifa lake la baadaye.