
Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group) imeshinda tuzo nne za Mwajiri Bora wa Mwaka 2017 (EYA) zinazotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), katika hafla ya iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
MeTL imeshinda tuzo hizo kupitia kampuni zake tanzu ambazo ni Mo Assurance Limited iliyoshinda kipengele cha Tuzo ya Kampuni Ndogo, 21st Century Holding Limited imeshinda nafasi ya pili ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Ndani na Star Oil Tanzania Limited imeshinda tuzo mbili, Tuzo ya Kampuni ya Kati na nafasi ya tatu ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Ndani.
Ushindi huo wa tuzo nne, umeiwezesha MeTL Group kuwa moja ya kampuni nne ambazo zimeshinda tuzo nyingi za ATE 2017, na kuwa kampuni ya kizalendo ambayo imeshinda tuzo nyingi kuliko kampuni zingine ambazo zimeshiriki katika tuzo hizo.

"Tuna furaha kushiriki kwenye tuzo za ATE 2017 na tuna furaha kushinda tuzo nne, naamini tumekuwa moja ya kampuni tano ambazo zimeshinda tuzo nyingi. Nafikiri sisi ni moja ya kampuni kubwa nchini na tunaendelea kukua na kugusa maisha ya watu wengi kila siku, ushindi kama huu utuwezesha kuongeza juhudi zaidi," alisema Dewji.
0 Comments