Ni wakati mwengine wa mwaka ambapo uvumi utaanza kusambaa. Uhamisho wa mwaka uliopita haukuwa na changamoto nyingi kutoka kwa timu sita bora katika ligi ya Uingereza huku timu zote za ligi hiyo zikitumia £215m mwezi Januari.
Wakati huu itakuwaje, Je timu kubwa zitagharamika kununua wachezaji?

Barani Ulaya...
Dirisha la uhamisho katika ligi tano kuu litafungwa kwa wakati mmoja .Dirisha la uhamisho la klabu za Uingereza, Ufaransa , Ujerumani , Itali na Uhispania litafungwa tarehe 31.
DIEGO LOPEZ (klabu: Espanyol; SafukipaUmri: 36)
DIEGO LOPEZ (klabu: Espanyol; Safu: kipa; Umri: 36)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionDIEGO LOPEZ (klabu: Espanyol; Safu: kipa; Umri: 36)
Anahusishwa na uhamisho wa :Crystal Palace.
Ni kipa anayejulikana kwa kupigania nafasi ya kipa na Iker Casillas katika klabu ya Real Madrid, alikuwa katika benchi wakati Reala Madrid iliposhinda kombe la vilabu bingwa 2014 na amekuwa mchezaji wa Ziada wa Espanyol kwa kipindi kirefu cha msimu. Pia aliichezea Villarreal, Sevilla na AC Milan.
KEVIN TRAPP (Paris St-Germain; kipa; 27)
Kevin TrappHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTrapp amiechezea Ujerumani mara mbili
Anahusishwa na uhamisho wa : Crystal Palace, Borussia Dortmund, Liverpool.
Mkufunzi wa PSG boss Unai Emery ana mpendelea sana kipa Alphonse Areola, na kipa raia wa Ujerumani Trapp ameanza kukerwa kutokana na ukosefu wa fursa ya kuiwakiulisha timu yake hususan wakati huu ambapo wachezaji wanajianda kuziwakilisha timu zao za kimataifa katika kombe la dunia
Anahusishwa na uhamisho wa: Manchester City, Liverpool, Napoli.
Beki wa kulia wa Croatia anadaiwa kutokuwa na furaha katika klabu ya Atletico Madrid, licha ya kutia saini mkataba wa miaka mitano wakati alipojiunga na timu hiyo mwaka 2016. Amejaribu kupigania kuiwakilisha timu yake katika kikosi cha kwanza huku mkufunzi Diego Simeone akimpendelea Juanfran.
DANIEL OPARE (Augsburg; Beki; 27)
DANIEL OPARE (Augsburg; Beki; 27)
Image captionDANIEL OPARE (Augsburg; Beki; 27)
Anahusishwa na uhamisho wa : West Ham, Stoke City, Everton, Swansea.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana ana uwezo wa kucheza kama beki wa kulia ama kushoto na anasakwa na baadhi ya vilabu vya Uingereza.Amekamilisha kandarasi yake na Augsburg na huenda klabu hiyo ya UJerumani inataka kumuuza.
LEON GORETZKA (Schalke; kiungo wa kati ; 22)
LEON GORETZKA (Schalke; kiungo wa kati ; 22)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLEON GORETZKA (Schalke; kiungo wa kati ; 22)
Anahusishwa na uhamisho wa: Manchester United, Arsenal, Barcelona.
Alikuwa katika kikosi cha Ujerumani kilichoshinda kombe la shirikisho ,Goretzka anafananishwa na kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Paul Scholes. Anakamilisha kandarasi yake mna yuko tayari kuondoka ili kupata changamoto mpya.
STEVEN NZONZI (Sevilla; kiungo wa kati; 29)
Steven N'ZonziHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionN'Zonzi amecheza zaidi ya mechi 200 katika soka ya Uingereza - akiwa Blackburn na Stoke
Anahusishwa na uhamisho wa: Everton, Arsenal.
Mchezaji huyo wa zamani wa Stoke na Blackburnalihusishwa na uhamisho wa kurudi katika ligi ya Uingereza baada ya kudaiwa kuzozana na mkufunzi wa zamani wa Sevilla Eduardo Berizzo, ambaye alifutwa kazi mnamo tarehe 22 Disemba. Uzoefu wake wa soka ya Uingereza kunaweza kumfanya kuwa kiungo muhimu.
ARDA TURAN (Barcelona; kiungo wa kati ; 30)
ARDA TURAN (Barcelona; kiungo wa kati ; 30)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionARDA TURAN (Barcelona; kiungo wa kati ; 30)
Anahusishwa na uhamisho wa : Arsenal, Trabzonspor.
Mchezaji huyo wa Uturuki hajaichezea Barcelona tangu mkufunzi Ernesto Valverde kuchukua usimamizi wa klabu hiyo. Ametngaza wazi kwamba anataka kuondoka Nou Camp mnamo mwezi Januari.
JEAN MICHAEL SERI (Nice; kiungo wa kati ; 26)
JEAN MICHAEL SERI (Nice; kiungo wa kati ; 26)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJEAN MICHAEL SERI (Nice; kiungo wa kati ; 26)
Anahusishwa na uhamisho wa : Barcelona, Manchester City, Liverpool.
Mchezaji huyo wa Ivory Coast alikuwa akiwindwa na Barcelona katika dirisha la uhamisho lililopita, lakini Nice ilikataa ombi la viongozi hao wa La Liga . Nice imaimarika baada ya kupata matyokeo mabaya , na huku uwezo wa klabu hiyo wa kufuzu kushiriki katika kombe la vilabu bingwa ukiwa mchache , Seri anaweza kutaka kuondoka mwezi Januari.
JAVIER PASTORE (Paris St-Germain; kiungo wa kati mshambuliaji ; 28)
JAVIER PASTORE (Paris St-Germain; kiungo wa kati mshambuliaji ; 28)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJAVIER PASTORE (Paris St-Germain; kiungo wa kati mshambuliaji ; 28)
Anahusishwa na uhamisho wa klabu za: Liverpool, Sevilla, Inter Milan.
Mchezaji mwenye kipaji ambaye hajathibitishiwa kuwa ataorodheshwa katika kikosi cha kwanza cha PSG , Pastore alitajwa kuwa mchezaji bora duniani na Eric Cantona, ambaye anasema angependelea iwapo Patore angesajiliwa na man United .Mchezaji huyo wa Argentina anapigiwa upato kuwa mchezaji muhimu katika kombe la dunia.
GELSON MARTINS (Sporting Lisbon; Winga; 22)
Anahusishwa na uhamisho wa : Liverpool.
GELSON MARTINS (Sporting Lisbon; Winga; 22)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionGELSON MARTINS (Sporting Lisbon; Winga; 22)
Sporting Lisbon inahitaji kitita kikubwa , na Martins anasemekana kuwa dau la kuondoka lakini mchezo wake katika ligi ya Ureno umevutia maoni yasio ya kawaida.
THOMAS LEMAR (Monaco; Winga/kiungo wa kati mshambuliaji; 22)
Thomas LemarHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLemar alihusishwa na uhamisho wa Arsenal katika dirisha la uhamisho lililopita
Anahusishwa na uhamisho wa : Arsenal, Chelsea, Liverpool.
NI miongoni mwa nyota wa klabu ya Monaco ilioshinda ligi msimu uliopita , na sasa ameorodheshwa katika kikosi cha Ufaransa ambapo amefunga mabao mawili dhidi ya Uholansi katika mechi ya kirafiki mnamo mwezi Novemba.
Arsenal na Liverpool zilijaribu kumsajili katika dirisha la uhamisho lililopita
HATEM BEN ARFA (Paris St-Germain; Winga/mshambuliaji /kiungo wa kati ; 30)
HATEM BEN ARFA (Paris St-Germain; Winga/mshambuliaji /kiungo wa kati ; 30)Haki miliki ya pichaMAGNUM PHOTOS
Image captionHATEM BEN ARFA (Paris St-Germain; Winga/mshambuliaji /kiungo wa kati ; 30)
Anahusishwa na uhamisho wa : Leicester City.
Baada ya msimu mzuri na Nice msimu uliopita 2015-2016, uhamisho wake hadi PSG haikuingiliana. Soka yake imekwama chini ya usimamizi wa Emery, ambaye haonekani kutakab kumpatia fursa ya kucheza katika kikosi cha kwanza. Meneja wa Ben Arfa's katika klabu ya Nice alikuwa Claude Puel, na huenda kuna uvumi kwamba huenda wakakutana tena katika klabu ya Leicester.