Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi mchungaji

wa
kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero huku akiwa sambamba na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali  wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa pamoja na madiwani wa chama hicho.
 Hili ndio kanisa la la Free Pentecost Church of Tanzania ambalo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia
chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa msaada wa mifuko ishirini na tano
(25) katika kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania lililopo kata ya
Isakalilo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa jipya ili kuendelea kutoa
huduma bora ya neon la mungu.



Akizungumza wakati wa ibada
iliyofanyika katika kanisani hilo Kabati alisema kuwa ni heri kujibembeleza kwa
mwenye mungu kuliko kujipendekeza kwa binadamu mwenzako hivyo ni bora kuchangia
shughuli za kihoro kuliko shughuli za kidunia.



“Mimi nimejitoa kuchangia
shughuli zote zinazo muhusu mungu hivyo naomba mnishirikishe nami nitakuja bila
kusita kwa kuwa ndio kazi yangu hata iliyonifanikisha mimi kuwa mbunge” alisema
Kabati



Kabati alisema kuwa aliwaahidi
kuwapa mifuko ishirini na tano ya saruji hivyo ametimiza ahadi hiyo kwa kuwapa
mifuko ya saruji yote aliyoiadi hivyo amefanikiwa kutekeleza na kuwaomba
wananchi wananchi wengine kuchangia maendeleo ya kanisani.



“Alikuja diwani hapa kwa niaba
yangu na kuahidi mifuko hiyo ambayo ni sawa na tani moja hivyo nimeamua
kutimiza kuwa lengo langu nikiahidi kitu lazima nitimize malengo yangu ya
kuitoa ahadi hiyo” alisema Kabati



Aidha Kabati aliwata wananchi
na viongozi mbalimbali kuendelea kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa jamii na
taasisi ambazo hazina uwezo wa kufikia mafanikio yanayotakiwa kwa ajili ya
kutatua kero zinazorudisha nyuma maendeleo.



Kabati amesema kuwa wananchi na
viongozi wanatakiwa kumtegemea mungu ili kuweza kufanikisha malengo wanayotarajia.



Katika hatua nyingine Kabati amewataka
wazazi kuwapeleka shule watoto wao ili wakapate elimu ambayo ndiyo itakuwa dira
ya maisha yao ya baadae.





Kwa uoande wake mchungaji wa
kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero alisema kuwa
walikuja viongozi wengi na kutoa ahadi nyingi lakini hakuna hata mmoja
aliyetimiza ahadi yake zaidi ya mbunge Ritta Kabati.



"Nilialika wageni wengi wakala
na kutoa ahadi nyingi kwa mbwembwe nyingi lakini kilichotokea hadi sana
viongozi wote hakuna aliyetimiza malengo hayo hivyo nichukue furasa kushukuru" alisema Okero



Mchungaji Okero alimshukuru
mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake ambayo itatusaidia katika ujenzi wa kanisa
letu