Meneja wa Chelsea Muitaliano,Antonio Conte, baada ya kichapo cha magoli 4-1 dhidi ya Watford amesema anaiachia klabu yake kufanya uamuzi kama wanafikiri hafanyi kazi nzuri.
Mabingwa hao watetezi wamepoteza michezo miwili mfululizo katika wiki na wako katika nafasi ya nne kwa alama 50.
"Nitabaki kuwa hapa na kujaribu kuifanya kazi yangu kwa nguvu zangu." Conte aliiambia BBC Radio 5
Muitaliano huyo alitwaa ubingwa wa ligi katika msimu wake wa kwanza, baada ya kufungwa na Bournemouth na Watford na sasa wako nyuma kwa 19 dhidi ya vinara wa ligi Manchester City.
Na kabla ya mchezo wa Jumatatu dhidi ya Watford, Conte aliomba sapoti ya uongozi na washabiki wa timu hiyo.
Baada ya mchezo wa jana Conte alisema "Nina fanya kazi na inatosha lakini klabu inaweza kutoa maamuzi mengine.
Conte amebakiza miezi 18 kabla ya kumaliza mkataba wake, alifafanua zaidi kwa kusema wachezaji wake walicheza huku wakiwa hawana utulivu na kama kocha anabeba msalaba wa lawama.
Kwa kuwa inawezekana alichagua kikosi kibaya cha kuanza mchezo huo nina kubali matokeo na tutapigana zaidi katika msimu huu.
0 Comments