Kiungo wa kati wa klabu ya Hull City nchini Uingereza Ryan Mason amelazimika kustaafu akiwa na umri wa miaka 26 kufuatia jeraha la fuvu la kichwa alilopata katika mechi dhidi ya Chelsea 2017.
Mason ambaye aliichezea Uingereza mara moja 2015 alilazimika kufanyiwa upasuaji baada ya kichwa chake kugongana na kile cha beki wa Chelsea Gary Cahill.
Uamuzi wake wa kustaafu unafuatia ushauri wa madaktari wa upasuaji wa neva.
Alianza kushiriki katika kandanda na klabu ya Tottenham na kujiunga na klabu ya Hull kwa dau la uhamisho £13m lililovunja rekodi katika klabu hiyo 2016.
Baada ya dakika nane ya matibabu uwanjani wakati wa mechi ya ligi ya Uingereza iliopigwa katika uwanja wa Stamford Bridge mwezi Januari 2016, Mason aliwekewa hewa alipobebwa katika machela na kutolewa uwanjani.
Alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya St Mary mjini London , ambapo alikaa kwa wiki moja na amezungumza kuhusu kuwa na bahati ya kuwa hai.
Mason alianza mazoezi na klabu hiyo tena mwezi Mei mwaka uliopita lakini hakuna tarehe ya yeye kurudi iliotolewa na baadaye mkufunzi wa klabu hiyo Leonid Slutsky alisema mwezi Agosti mwaka uliopita swali sio kuhusu soka bali kuhusu maisha yake wakati mchezaji huyo alipokutana na mtaalam wa tatu.
Klabu ya hull City imewashukuru wale wote waliomsaidia kupona katika kipindi cha miezi 12 iliopita.
|
0 Comments