Viongozi wawili wa upinzania walikua wamepigwa marufuku kusafiri kwa ndege hadi Zimbabwe kuhudhuria mazishi ya Morgan Tsvangirai
Senator James Orengo na mkuu wa masuala ya fedha wa Muungano wa Upinzani nchini kenya ( NASA) Jimi Wanjigi wamepanga kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai.

Lakini maafisa walisema kuwa wawili hao walishindwa kuwasilisha amri ya mahakama ya kubadilisha uamuzi wake wa sasa wa kuharamisha paspoti zao.
kwa pamoja Orengo na Wanjigi ni wafuasi sugu wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ambaye alijitangaza mwenyewe kama "rais wa watu" mwezi uliopita.
Kunma hofu kwamba serikali inapuuza uhuru wa raia kujibu hatua ya Bwn. Odinga kuapishwa
Tofauti na Bwn. Orengo na Bwn. Wanjigi, Odinga aliruhusiwa kuondoka kwa ndege hadi Zimbabwe, bila matatizo yoyote, kwa mazishi ya Bwn. Tsvangirai, ambae alikua rafiki yake wa muda mrefu.
Mwanasiasa huyo wa upinzani wa Zimbabwe alifariki dunia kwa maradhi ya saratanio ya utumbo tarehe 14 Februari, na maelfu ya watu wamehudhuria mazishi yake katika kijiji cha Buhera.
Jeneza la hayati kiongozi wa upunzani Morgan Tsvangirai ikibebwa ndani ya kanisa la kimethodisti Mabelreign mjini Hararekwa ibada ya wafu Februari 18, 2018.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMazishi yamefanyika ya Tsvangirai yamefanyika katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare Jumatatu,
Maafisa wa uhamiaji nchini Kenya walimzuilia Bwana Orengo na Bwana Wanjigi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumatatu
Jumanne , Bwana Kihalangwa alituma ujumbe wa Twitter kwamba hatimae amri ya mahakama imefika na wawili hao wameruhusiwa kuondoka kuelekea Zimbabwe
Bwn. Orengo alipinga ujumbe wa Bwn. Kihalangwa, akisema kuwa maafisa wa uhamiaji walipokea amri ya mahakama Jumatatu usiku.
Na kwamba yeye na Bwn. Wanjigi karibia wanakaribia kuondoka kuelekea Zimbabwe baadae Jumanne.
IKatika wiki za hivi karibuni, serikali ya Kenya imekuwa ikiwakamata viongozi wa upinzani wafuasi wa Bwn. Odinga.