Korea Kaskazini ina nia ya kufanya mazungumzo na Marekani, kwa mujibu wa Korea Kusini.
Tangazo hilo limekuja baada ya Jenerali Kim Yong-Chol kukutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, kabla ya sherehe za kufungwa kwa mashindano ya olimpiki wa msimu wa baridi.

Binti ya rais wa Marekani Donald Trump Ivanka pia alihudhuria sherehe hizo, lakini maafisa wa Marekani wamekana kufanya mkutano na ujunbe kutoka Korea Kaskazini.
South Koreans protest against Gen Kim Yong-chol's visit in Paju, South Korea. Photo: 25 February 2018Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionWaandamanaji wa Korea Kusini waliandamana kupinga ziara ya Kim Yong-Chol
Marekani inasema Korea Kaskazini ilijiondoa kutoka kwa mkutano na Makamu wa Rais Mike Pence wakati wa sherehe za ufunguzi.
Eneo la rasi ya Korea limegawanyika tangu vita vya mwaka 1950 hadi 1953 na pande hizi mbili hazijawai weka sahihi mkataba wa amani.
Uhusiano baina ya Korea Kaskazini na Kusini umeonekama kama njama ya Korea kuvuruga ukaribu kati ya Korea Kusini na Marekani.
US Vice-President Mike Pence in front of North Korea's Kim Yong-nam (C) and Kim Yo-jong (R)Haki miliki ya pichaPOOL
Image captionMarekani inasema Korea Kaskazini ilijiondoa kutoka kwa mkutano na Makamu wa Rais Mike Pence wakati wa sherehe za ufunguzi
Hata hivyo wataalamu wanaonya kuwa yanayofanaika sasa hayamalizi kikomo misukosuko ya kieneo hasa kufuatia majaribio ya nyuklia na ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini.
Siku ya Ijumaa Marekani ilitangaza awamu mpya ya vikwazo dhidi ya korea Kaskazini.