Wadau wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ((COSTECH) Dar es Salaam jana.
Mkutano ukiendelea.
Dk.Richard Mbunda kutoka UDSM, akielezea changamoto mbalimbali zitokanazo na matumizi ya mbegu za GMO katika kilimo.
Usikivu katika mkutano huo.
Dkt. Aloyce Kulaya akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Dkt. Adolphine Kateka akichangia.
Dkt. Goodluck Ole Medeye, akielezea umuhimu wa mbegu hizo katika kilimo.
Alfred Mmbaga kutoka Tanzania Meat Board akichangia mada.
Elisa Greebe kutoka Chuo Kikuu cha Leeds akichangia.
Mkulima mdogo Ernest Likoko akichangia mada.
Dk Emmarold Mneney akichangia mada kwenye mkutano huo.
Emma Nyerere kutoka Taasisi ya Pawo Pan African Women Organisation Tanzania akichangia jambo.
Dkt. Nicholous Nyange, akizungumza kwenye mkutano huo.Mada zikichangiwa. |
Dkt.Roshan Abdallah kutoka Agricultural Innovation Research Foundation Tanzania, akichangia jambo.
Na Mwandishi Wetu
WASHIRIKI wa Kavazi la kwanza la Mwalimu Nyerere kwa mwaka 2018 wameomba elimu zaidi itolewe kwa jamii ili kusaidia kuwa na uelewa wa pamoja kama nchi katika kuelekea kutumia teknolojia ya uhandisi jeni kukablina na changamoto zinazomkabili mkulima nchini kwa sasa na kuinua tija.
Wakichangia mjadala huo uliolenga kuangalia nafasi ya mbegu za GMO na teknolojia ya uhandisi jeni katika kilimo wadau hao kutoka sekta na taasisi mbalimbali nchini wamesema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na watafiti kwa kushirikiana na serikali na makampuni mengine ya nje jamii inahitaji kuelimishwa ili kuondokana na mashaka ambayo yamekuwa yakizunguzwa na baadhi ya wadau kuhusu mbegu hizo.
Wamesema wakulima wengi uzalishaji wao ni mdogo kutokana na kutumia zana duni,kutozingatia kanuni bora za kilimo,Mbegu zisiszo bora na teknolojia zingine ambazo zimewafanya wakulima kuendelea kubaki palepale na kuona kilimo sio kazi yenye tija na thamani kama kazi zingine na hivyo wadau hao kuomba mjadala mpana ufanyike wa kitaifa kuhusu teknolojia ya GMO na kuona kama ina mchango katika kusaidia kumkomboa mkulima kutoka katika hali yake ya sasa.
Akizungumzia umuhimu wa mbegu hizo za GMO kwa taifa na wakulima nchini aliyekuwa (Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika serikali ya awamu ya nne) ????? Dkt. Goodluck Ole Medeye alisema kuwa mchakato wa kuanza au kutokuanza kutumia mbegu za GMO ulianza zamani lakini serikali kupitia waalamu wake walikaa chini na kutathimini uhitaji wa teknolojia hiyo na kuona kuwa ni mkubwa na hivyo kuamua kuwapa nafasi watafiti kufanya kwanza utafiti ili kujiridhisha juu ya faida na hasara zake.
Alisema kuwa yeye binafsi alikuwa mtu wa kwanza kupinga matumizi ya mbegu zinazotokana na teknolojia hiyo lakini baada ya kuwapa nafasi watafiti kueleza na kuwaelimisha mawaziri na viongozi wengine wa serikali aliona kuwa hakuwa sahihi na kwa pamoja wakafikia uamuzi wa kuwaruhusu watafiti wafanye utafiti nchini ili kujiridhisha kuwa na uwezo wa kutambua mbegu na bidhaa zitokanazo na teknolojia hiyo.
Dkt. Medeye aliongeza kuwa hakuna namna ambayo Tanzania itakwepa kutumia mbegu hizo au bidhaa za GMO kwakuwa Tanzania sio kisiwa kama nchi zinazoizunguka Tanzania zinafanya tafiti kwa kasi na kutumia mbegu hizo basi Tanzania itajikuta wananchi wake wanatumia mbegu hizo kwani kwa sasa nguo nyingi tunazovaa zinatoka nchi zinazozalisha pamba ya GMO na baadhi ya vyakula tunavyokula kutoka nje vinatokana na mbegu za GMO.
Waziri huyo wa zamani amebainisha kuwa wakulima wengi wa Tanzania kwa miaka nenda rudi bado wanazalisha chakula kidogo sana ambacho hakikidhi mahitaji ya kaya zao na kupata ziada kwaajili ya kuuza kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo zana dunia,kutotumia mbinu bora za kilimo na hasa mbegu bora hivyo ni wakati sasa nchi ikaona umuhimu wa kumuinua mkulima kwa kumpatia mbegu zenye kumletea matumani na tija.
Kwa upande wake mtafiti mstaaafu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ((COSTECH) Dkt. Nicholous Nyange ambaye alikuwa mtafiti kwenye masuala ya tafiti za bioteknolojia za kilimo nchini aliyewasiliasha mada juu umuhimu wa teknolojia na mbegu za GMO amesema kuwa inakadiriwa kuwa Tanzania kwa sasa inawatu wapatao milioni 58 na idadi hii inaongezeka kila siku na kama sayansi haitatumika kusaidia kuzalisha chakula cha kutosha basi huenda taifa likasumbuliwa na njaa kila mwaka kwenye maeneo mengi.
Alisema wakulima pamoja na jitihada kubwa zinaofanywa na wakulima kulima na kupanua mashamba kila siku lakini bado hawajaweza kuzalisha chakula cha kutosha kutokana nasababu mbalimbali ikiwemo wadudu,magonjwa na changamoto zingine zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Ukame kwenye maeneo mengi ya nchi kwa sasa.
Dkt,Nyange amesema kawimu zinaonyesha kuwa Tanzania kwenye uzalishaji wa mahindi unakadiriwa kufikia ati ya tani 1.5 hadi tani mbili pale ambapo hali ya hewa na mtawanyiko wa mvua utakuwa mzuri lakini kwa nchi zilizoendelea kama vile marekani wanazalisha tani 8 hadi 9 kwa ekari kutokana na kutumia teknolojia za kisasa ili kuongeza uzalishaji .
Alisema kuwa pamoja na uchumi wa taifa kukua kwa silimia 7 lakini kilimo ambacho ndio uti wa mgongo wa mtanzania ambao zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wanakitegemea chenyewe kinakua kwa asilimia 3 tu na hivyo kusema kuwa kama teknolojia ikitumika na wakulima wakawezeshwa kilimo kitaweza kuchangia vyema kwenye pato la taifa na kuwanufaisha wakulima ambao tunaona TASAF inawapa fedha kupitia mpango wa serikali wa kusaidia kaya masikini.
Aliongeza kuwa eneo linalofaa kwa kilimo na makazi likigawanywa kwa idadi ya watu waliopo nchini katika kipindi kifupi kichacho halitatosha kupata maeneo ya kutosha kwaajili ya kilimo makazi na shughuli zingine za kibinadamu hivyo njia pekee ni kuwawezesha wanananchi na wakulima kutumia mbinu za kisasa kuzalisha kwa wingi kwenye maeneo madogo ili kuendana na ongezeko la idadi ya watu na eneo la nchi lililopo ambalo haliongezeki.
Kwa upande wake Dkt. Aloyce Kulaya mtafiti wa zao la mahindi mstaafu na mshauri wa mradi wa Water efficient Maize for Africa (WEMA) alisema kuwa suala la GMO linaangalia tuu kwenye vyakula lakini teknolojia hiyo inatumika zaidi kwenye kutengeneza madawa kama yale ya kisukari na kubainisha kuwa hata kama dawa ya ukimwi ikipatikana basi inaweza kuwa kwa kutumia njia hii pekee na sio nyingine.
Alisema teknolojia ya uhandisi jeni sio ndio njia pekee ya kupata ufumbuzi wa matatizo ya wakulima lakini pale mbinu za kawaida zinaposhindwa ndio teknolojia hiyo pekee hutumika katika kupata ufumbuzi wa haraka na sahihi wa changamoto za magonjwa,ukame na wadudu ambazo zinawasumbua wakulima nchi nzima ambayo binu za kawaida zimeshindwa.
Dkt. Kulaya aliongeza kuwa kwa wasiwasi wa watu kuwa mbegu za asili zitapotea hauna maana kwakuwa mbinu hizo za kuupatia mmea kinga na uwezo wa kuwa na sifa fulani kunaweza kufanyika pia kwenye mbegu zetu za asili na hivyo kuziwezesha mbegu hizo kuhimili magonjwa,wadudu na changamoto zingine na kumuwezesha mkulima kupata mazao ya kutosha.
Kwa upande wake Profesa, Rwaitama ameitaka serikali kuwezesha vituo vyetu vya utaifa nchini kuwa na uwezo wa kufanya tafiti hizi ambazo zinaweza kusaidia kuwainua wakulima kupambana na changamoto zinazowakabili badala ya kutegemea wafadhili pekee ambao wanapoleta fedha kwenye utafiti Fulani wanakuwa na vigezo vyao na sio lazima view kipaumbele cha nchi.
Alisema vituo vingi vya utafiti vya zamani vilikuwa vinafanya kazi nzuri katika kazi za utafiti lakini kwa sasa vimeshuka utendaji wake na kuonekana kuwa na mchango mdogo sana kwa maendeleo ya nchi ili kuweza kuwa na udhibiti wa kile kinachozalishwa kuwa mali ya taifa kwakuwa kitakuwa kimezalishwa kwa kutumia fedha za wananchi.
Prof. Rwaitama akitolea mfano wa utafiti wa Panya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) alisema ni moja ya matunda makubwa ambayo yanaipatia Tanzania na watafiti wake heshima kubwa katika kutumia panya kufanya kazi mbalimbali kubwa duniani kama vile kutambua mabomu,makohozi ya TB kwa haraka.
Naye Mwenyekiti wa mkutano huo Dkt. Ng’wanza Kamata ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) alisema kuwa Kavazi la Mwalimu Nyerere litaendelea kufanya mijadala juu ya jambo hili kila mara ili kusaidia kuwepo kwa mjadala mpana katika kujadili faida na hasara za teknolojia ya Uhandisi jeni kabla teknolojia hiyo haijamfikia mkulima.
Alisema wananchi wote wakielewa vizuri jambo hili litasaidia kuondoa mashaka juu ya usalama wa teknolojia ambao umekuwa ukitolewa na watu mbalimbali na mashaka hayo yakiondoka ndipo sasa kila mtu anaweza kuwa huru kuchagua kuitumia teknolojia hiyo au la kwa manufaa yake na manufaa ya taifa kwa ujumla.
Profesa, Kamata aliongeza kuwa mashaka ni lazima kwa jambo lolote au teknolojia yoyote mpya inapoingia sokoni na huu ndio wakati muafaka wa watafiti kusikia mashaka na watu na kisha kuyatafutia majibu ya kisayansi kwani hakuna mtu anayeweza kufurahia jambo bila kuwa na wasiswasi hususani kwa teknolojia mpya yoyote.
Awali akiwasilisha mada yake ambayo ilitakiwa kujibiwa na Dkt. Nyange dhidi ya GMO mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaamu, Richard Mbunda alisema bado kuna taarifa ambazo zinapishana katika kiwango ambacho mbegu za GMO zinazostahimili ukame ambazo zinefanyiwa majaribio kwenye kituo cha utafiti wa kilimo makutupora katika uwezo wake wa kupunguza hasara kwa mkulima.
Mbunda amesema mashaka makubwa wanayoyaona baadhi ya watu ni kuhusu usalama wa vyakula vinavyotokana na mbegu za GMO kama chakula kwa maana ya afya na mazingira mambo ambayo ni lazima watafiti wayaangalie na kujiridhisha kabla ya kuzipeleka mbegu hizo kwenye mamlaka za serikali zinazopitisha mbegu zote nchini.
Mtoa mada huyo alieleza wasiswasi wake na kutaka kujua juu ya namna mkulima mdogo atakavyoweza kunufaika na teknolojia hiyo ili isijemfanya mkulima kuwa mtegemezi wa mbegu kutoka nje ya nchi na kutaka kujua namna wakulima watakavyoweza kupata mbegu hizo kwa urahisi na bei nafuu pale ambapo zitapitishwa na kuwa mbegu ili kutumika hapa nchini.
0 Comments