Maafisa sita wa polisi wamekamatwa kuhusiana na kifo cha mwanafunzi wa chuo cha kitaifa cha usafirishaji Akwilina Akweline.
Hayo ni kwa mujibu wa kamanda wa sehemu maalamu mjini Dar es Salaam Lazaro Mambosasa wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika siku ya Juamapili.

Mambosasa pia alibaini kwamba maafisa wa polisi wanachunguza maafisa wengine 40 kuhusiana na kifo hicho.
Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa mwaka wa kwanza katika chuo hicho ambaye jina lake lilisambazwa katika mitandao ya kijamii aliripotiwa kupigwa risasi alipokuwa ndani ya basi siku ya Ijumaa.
Shirika la wanafunzi nchini limemtaka waziri wa maswala ndani nchini humo Mwigulu Nchemba kuchukua jukumu la kisiasa na kujiuzulu kufuatia kisa hicho.
Akizungumza na wanahabari, mwenyekiti wa shirika hilo Abdul Nondo alisema kuwa iwapo Mwigulu hatojiuzulu basi watamtaka rais John Pombe Magufuli kumfuta kazi.
''Kufuatia mauaji na kutoweka kwa watu kadhaa ni wakati kwamba bwana Mwigulu anafaa kuchukua jukumu na kujiuzulu'', alisema.
Wakati huohuo Serikali imesema kuwa itagharamika kusimamia mazishi ya mwanafunzi huyo.
Marehemu Akwilini AkwilineHaki miliki ya pichaPAUL WILLIAM SABUNI
Image captionMarehemu Akwilini Akwiline
Akizungumza mjini Dar es Salaam waziri wa elimu, Sayansi na Teknolojia Joyce Ndalichako alisema kuwa Akwilina aliuawa wakati alipokuwa akielekea Bagamoyo.
''Aliuawa alipokuwa akielekea Bagamyo kuwasilisha ombi lake la kutaka kupewa mafunzo kwa vitendo'', alisema.
Kwa upande wake naibu waziri wa maswala ya Tanzania Hamad Masauni amesema kuwa serikali itahakikisha kuwa uchunguzi kuhusu kisa hicho unafanyika mara moja ili washukiwa washtakiwe.