RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali
Mohamed Shein amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mapinduzi kwa
kuongeza Wizara moja zaidi, na kuwabadilisha Wizara baadhi ya Mawaziri.
Kufuatia
mabadiliko hayo, shughuli za Vijana zimehamishiwa katika Wizara mpya ya
Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo; shughli za Mazingira zimehamishiwa
katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais;na shughli za Wakala wa Serikali
wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya
Kale.
Aidha, amewateua Naibu Mawaziri wapya wawili na
kumbadilisha Wizara Naibu Waziri mmoja. Kufuatia mabadiliko hayo,
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa itakuwa na Wizara 14 zenye
Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:
1. OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
i. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi- Mheshimiwa Issa Haji Ussi Gavu
2. OFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NAUTAWALA BORA
i. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman
ii. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Khamis Juma Mwalim
3. OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ
i. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Haji Omar Kheri
ii.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa
na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Shamata Shaame Khamis
0 Comments