KITUO cha kufua umeme mkoani Rukwa kimepata jenereta  ya
kufua umeme yenye uwezo  wakuzalisha MegawatI 10 zitakazoimarisha
uzalishaji wa umeme mkoani humo.
Akizungumzia ujio wa jenereta hiyo, Meneja wa TANESCO Mkoani

Rukwa Bw.Herini Muhina, alisema, hali ya uzalishaji umeme itakuwa bora zaidi
na hivyo kufanya upatikanaji wa umeme katika wilaya za Sumbawanga, Laila,
Kalambo na Nkasi kuwa bora zaidi.

“Nimatumaini yetu kuwa ongezeko hilo la umeme, litasaidia kwenda sambamba na
mipango ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda kwani umeme wa uhakika
utakuwepo na hivyo kufanya Mkoa wa Rukwa kuwa sehemu nzuri ya kuwekeza kwenye
sekta hiyo ya viwanda.” Alitoa hakikisho Bw. Muhidin.


  Kaimu Meneja Mkuu Rasilimali Watu wa TANESCO Makao Makuu, Bw. Nathan Daimon (watatu kushoto), akipta maelezo kutoka kwa mdhibiti na mwendeshaji mifumo ya umeme wa Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO), kituo cha Sumbawanga Mkoani Rukwa Bw.Halfan R. Seba
 kuhusu jenereta ujio wa jenereta yenye uwezo wa kuzalisha umeme Megawati
10 kwenye kituo hicho.


Bw. Daimon akipewa maelezo zaidi ya uendeshaji shughuli za TANESCO mkoani Rukwa.
 


 
NA SAMIA CHANDE,
SUMBAWANGA