Serikali ya Ethiopia imewasamehe wafungwa 746, akiwemo mwandishi wa habari maarufu Eskinder Nega, chombo cha habari cha serikali Fana Broadcasting Corporation, FBC kiimeripoti kwenye mtandao wake.
Eskinder alihukumiwa kifungo cha miaka 18 mwaka 2012 baada ya kushutumiwa kuwa na mahusiano na kundi cha upinzani lililo na makazi yake nchini Marekani ambalo serikali ya Ethiopia inalichukulia kama kundi la kigaidi.
Mwanasiasa wa upinzani Andualem Arage, aliyehukumiwa pamoja na Eskinder pia amesamehewa, imeripoti FBC
Alipokuwa mfungwa, Eskinder alitwaa tuzo mashuhuri wa Pen America 'Uhuru wa kuandika" kwa kuchapisha habari zilizokosoa rekodi ya haki za binadamu ya Ethiopia.
Pen America ilimpongeza Eskinder kwa kuwa kipaumbele kwa kupigania uhuru wa vyombo vya habari na alifungiwa jela kwa "kukiuka sheria za kupinga ugaidi baada ya kuikosoa serikali kwa kuwakamata waandishi wa habari wa na wanaharakati"
Wafungwa hao 746 ni miongoni wafungwa wa mwisho waliosamehewa tangu serikali ilipoahidi kuwaachilia wafungwa kwa jithada za kuchochoea maridhiano kwenye nchi iliyokuwa na migogoro tangu 2015.
Mwezi uliopita kinara wa upinzani Merera Gudina aliachiliwa kutoka gerezani.
Hata hivyo, maandamano ya kupinga serikali yameendelea kaskazini mwa Ethiopia.
Waandamanaji wanahisi mabadiliko hayajaweza kufikia na kumaliza miongo miwili ya malalamiko ya unyanyapaa wa kiuchumi na kisiasa.
|
0 Comments