Mahakama nchini Iraq imewahukumu kifo wanawake 15 raia wa Uturuki, baada ya kupatwa na hatia ya kujiunga na kundi la Islamic State.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa wanawake 15 walipewa hukumu ya kifo, na wengine wakahukumiwa kifungo cha maisha.
Wanawake hao walikiri kuolewa na wapiganaji wa Islamic State au waliwasaidia kufanya mashambulizi ya kigaidi.
Maelfu ya raia wa kigeni wamepigana na kuuliwa wakipigana na IS nchini Iraq na Syria.
Serikali ya Iraq imatangaza kumalizika kwa vita vyake na kundi hilo mwezi Disemba. Licha ya IS kutimuliwa kutoka ngome zake kuu, kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga na mashambulizi mengine.
Wanawake hao wanaotajwa kuwa kati ya umri wa miaka 20-50, walikuwa wamevalia nguo nyeusi wakiwa mahakamani mjini Baghdad siku ya Jumapili. Wanne walikuwa na watoto wadogo.
Mmoja alimuambua jaji kuwa alikuwa amewapiga vita wanajeshi wa Iraq akiwa na IS.
Takriban wanawake 560 na watoto 600 wamezuiliwa nchini Iraq kwa kushukiwa kuwa wapiganaji au jamaa za wapiganaji wa IS.
Mapema mwezi huu mwanamke raia wa Uturukialikuhukumiwa kifo na wengine 10 wakahukumiwa kifungo cha maisha jela.
|
0 Comments