WAZIRI Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn amejizulu. Mwanasiasa huyo pia amejiuzulu uenyekiti wa chama cha People's Revolutionary Democratic Front (EPRDF).
Hailemariam leo amewasilisha barua ya kujiuzulu ikiwa imepita miaka mitano tangu aanze kuiongoza nchi hiyo baada ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Meles Zenawi mwaka 2012.
“Vurugu na mgogoro wa kisiasa vimesababisha vifo na wengi kuyahama makazi yao” amesema wakati akizungumza kupitia televisheni ya taifa.
Mamia ya watu wamekufa wakati wa maandamano ya kuipinga Serikali.
“Naona kujiuzulu kwangu ni muhimu katika azma ya kufanya mageuzi yatakayowezesha kupatikana kwa amani na demokrasia endelevu” amesema.
Maandamano hayo yalianza mwaka 2015 kwenye mikoa ya Oromia na Amhara na baadaye yakasambaa kwenye maeneo mengine nchini humo.
0 Comments