Mwalimu kutoka Ghana alivuma mtandaoni baada ya kuweka picha akichora programu ya Microsoft Word kwenye ubao wakati wa darasa la tarakilishi.
Baada ya picha yake Owura Kwadwo kusambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter, kampuni ya Microsoft ilivutiwa na mwalimu huyo na kumsifia kwa jitahada zake za kuwafundisha wanafunzi wake.
Mmoja ya tweet ikisema "Darasa la teknohama Ghana. Hamna Kompyuta? Hamna Shida."
Kujitoa kwake kwa dhati kuliwavutia sana wafanyakazi wa Microsoft, waliandika kwenye akaunti yao ya Twitter, kuwa Bw. Kwadwo atapewa msaada wa vifaa vya kumsaidia katika kazi yake.
Bw Kwadwo aliweka picha hizo wiki mbili zilizopita kwenye ukurasa wake wa Facebook kuonesha hali halisi ya kufundisha darasa la somo la kompyuta bila kuwa na kompyuta yenyewe.
Alisema "kufundisha somo la kompyuta nchini Ghana inachekesha. Kompyuta ni ubao. Ninawapenda wanafunzi wangu , kwa hiyo nitajitahidi niwaeleweshe"
0 Comments