Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
SERIKALI imetoa miezi mitatu kwa Maofisa elimu wa mikoa kuhakikisha wanaondoa mlundikano wa wanafunzi madarasani hasa waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichakoalipokuwa akifunga kikao kazi cha Makatibu Tawala Wasaidizi wa Elimu na Mipango ngazi ya Mikoa, Wakaguzi wa ndani wa kutoka Halmashauri zote 186 Tanzania Bara, mjini hapa.

wamefanya vibaya katika uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza na kusababisha darasa moja kuwa na wanafunzi zaidi ya elimu anayefuata miongozo yetu inayotaka darasa moja kuwa na wanafunzi 40, na unajua miundombinu ilivyo inakuwaje unafanya uchaguzi watoto 200 wanaenda kukaa darasa moja… nina taarifa za baadhi ya wanafunzi wa sekondari wanasomea nje, nikasema siendi huko kwani hilo ni kosa la kiholela, nawapa miezi mitatu mkashughulikie hili,” alisema.
watashindwa kushughulikia tatizo la mlundikano wa wanafunzi, atapeleka majina yao kwa Waziri Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ili awachukulie hatua. Profesa Ndalichako alisema uchaguzi wa wanafunzi unategemea nafasi na miundombinu iliyopita na si kwa kila aliyefaulu achaguliwe na kusisitiza mlundikano ndani ya darasa haukubaliki.Aidha, aliagiza shule zote za kidato cha tano ambazo hazijasajiliwa zikaguliwe na zilizokidhi viwango zisajiliwe ili zipokee wanafunzi wa kidato cha tano.
Alisema pia serikali itaendelea kutatua changamoto zinazowakabili maofisa hao ikiwemo suala la usafiri na kwamba katika kuhakikisha kunakuwepo na usimamizi kwenye taaluma, serikali imeagiza pikipiki 2,800 kwa ajili ya waratibu elimu kata. Awali, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tamisemi (ELIMU), Tixon Nzunda alisema katika kikao maofisa hao wameahdi kufuta ziro kwenye shule za umma.