Shambulio la ufyatulianaji wa risasi la Las Vegas lilikuwa la kwanza katika utawala wa kiongozi huyo wa Marekani.
Baada ya mtu mmoja kujificha katika hoteli ya Manadalay Bay na kuwafyatulia risasi kwa dakika 10 watu waliokuwa wakielekea katika tamasha , na kuwaua makumi ya watu huku mamia wakijeruhiwa , rais Trump alielekea Vegas na kukutana na familia, mashahidi , maafisa wa matibabu na huduma za dharura.

Aliondoka katika ndege ya Air Force One akihisi kwamba siku ilikwisha ilivyokuwa kutokana na hali iliokuwepo.
Lakini muda mfupi tu baada ya kuwasili mjini Washington ,hisia zake zilibadilika mara moja.
Na kulikuwa na sababu mbili.
Ziara yake ya Vegas haikutangazwa katika runinga kadhaa. Lakini ya pili ni kwamba habari kuu ilikuwa inasema kuwa Rex Tillerson alikataa kukana kwamba alimuita Donald Trump 'Mjinga'.
Rex Tillerson alidaiwa kumuita rais Trump 'mjinga' katika mkutano wa pentagon
Image captionRex Tillerson alidaiwa kumuita rais Trump 'mjinga' katika mkutano wa pentagon
Waziri wa maswala ya kigeni alikuwa katika mkutano katika idara ya ulinzi wakati alipotoa tamko hilo kuhusu rais Trump. Hayo ndio maswala ambayo huwezi kuyafutilia mbali kwa urahisi.
Huyu ni rais ambaye anayapatia kipau mbele maswala yote yanayokumba serikali yake hivyobasi tangu wakati huo 'chuma cha Tillerson kilikuwa kimotoni'.
Ni watu wawili ambao hawalingani kibiashara licha ya kuwa wote wamekuwa wafanyibiashara wakubwa. Trump amekuwa akifanya biashara za malkia wa Urembo huku Tillerson akishughulikia biashara za mafuta na kemikali. Lakini ,mbali na hilo wamekuwa watu wawili tofauti .
Ni aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni wa zamani Condoleezza Rice aliyempendekezea bwana Trump, Rex Tillerson na aliyekuwa mkurugenzi wa Ujasusi CIA Robert Gates.
Walidhani ana uzito na uzoefu wa kufanyia kazi kampuni kubwa ya Exxon na mtu atakayewakilisha maslahi ya Marekani na kuitetea kote dunini.
Waandamanaji wakibeba mabagno yalioandikwa kampuni ya #exxonknewHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUteuzi wa Tillerson ulipingwa na wengine
Na wakati wote huo hakuonekana kuwa mkakamavu katika kazi yake.
Mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov ulifanyika vizuri huku wote wawili wakionekana kuwa wakakamavu na mawaziri wasiopenda mchezo.
Na alikuwa na mangi ya kuogopesha huku akipunguza matumizi ya wizara hiyo bila mkakati wa kuidhinisha mipango yake.
Idara ya maswala ya kigeni ya Marekani ilikuwa imekosa mwelekeo huku wafanyikazi wa vyeo vya chini wakijipatia majukumu makubwa kwa kuwa vyeo vya juu vilikuwa havina maafisa walioajiriwa.
Ilikuwa hali ya kukosa mwelekeo. Na baadaye kulikuwa na Donald Trump. Wacha tamko la mjinga - hawa ni watu wawili ambao hawakuelewana kibinafsi na pia kisera.
Mara kadhaa rais Trump alimpuuza waziri wake wa maswala ya kigeni. Kuhusu Korea Kaskazini ,rais Trump alichapisha ujumbe katika mtandao wa Twitter kwamba Tillerson alikuwa akipoteza muda wake.
Kuhusu maswala mengine alituma watu wa familia yake kwenda kufanya majadiliano ughaibuni. Kulikuwa na hisia kwamba Rex Tillerson alikuwa afisini lakini hakuwa na uwezo.
Rais Trump muda mfupi baada ya kumfuta kazi Rex Tillerson
Image captionRais Trump muda mfupi baada ya kumfuta kazi Rex Tillerson
Alionekana kama afisa ambaye hakuambatana na kazi yake , akisafiri duniani kwa kutumia cheo dhana , lakini hakuwa na ushawishi wowote wa kubadilisha fikra za rais.
Hadharani alijionyesha kuwa mwaminifu na kufanya kazi kana kwamba alikuwa akijua kilichokuwa kikiendelea wakati ambapo ilikuwa kinyume na yaliokuwepo.
Isipokuwa jana usiku, alipokuwa akirudi nyumbani kutoka ziara ya Afrika, alikuwa kama kawaida . Alizungumzia kuhusu kile kilichotokea Salsbury Uingereza ambapo jasusi wa Urusi na mwanawe wa kike waliwekewa sumu ya kuharibu neva kutoka Urusi.
Mahala ambapo Ikulu ya Whitehouse haikutoa lawama zozote kuhusu Urusi , Tillerson aliingilia kati . Pengine aligundua kwamba 'chuma chake kilikuwa kweli motoni' pengine hakujali tena na alipokuwa katika ndege akafutwa kazi.
Tillerson aliwasili katika uwanja wa ndege wa kambi ya jeshi ya Andrews ambapo mfanyikazi wake mmoja alimuelezea kwamba rais Trump amechapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amefutwa kazi.
Image captionTillerson aliwasili katika uwanja wa ndege wa kambi ya jeshi ya Andrews ambapo mfanyikazi wake mmoja alimuelezea kwamba rais Trump amechapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amefutwa kazi.
Na mwisho huo ulikuwa mfano kamili wa uhusiano uliokuwepo kati ya wawili hao. Wawili hao wenye misimamo tofauti ya kisiasa walifanya kazi pamoja kwa muda mrefu.
Walikuwa watu wenye hasira za viwango tofauti ,tabia na mitindo ya kutekeleza wajibu wao. Tillerson aliwasili katika uwanja wa ndege wa kambi ya jeshi ya Andrews ambapo mfanyikazi wake mmoja alimuelezea kwamba rais Trump amechapisha ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba amefutwa kazi.
Kwa sababu Tillerson hayuko katika mtandao wa Twitter , ujumbe huo ulilazimika kuchapishwa. Na majibu ya Trump alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mapema alfajiri alisema: Nadhani Rex atafurahi sana... sasa nina hakika.
Orodha ya maafisa wa serikali ya Marekani waliofutwa kazi na rais Donald Traump au wakajiuzulu tangu achukue mamlaka.
  1. Rex Tillerson, waziri wa maswala ya kigeni - 13 Machi 2018
  2. Gary Cohn, Afisa mkuu wa maswala ya kiuchumi - 6 Machi 2018
  3. Hope Hicks, MKurugenzi wa mawasiliano Ikulu ya Whitehouse - 28 Februari 2018
  4. Rob Porter, Katibu katika Ikuku ya White House- 8 Februari 2018
  5. Andrew McCabe, Naibu mkurugenzi shirika la FBI - 29 Januari 2018
  6. Tom Price, Waziri wa afya - 29 Septemba 2017
  7. Steve Bannon, Afisa mkuu wa mipango - 18 Agosti 2017
  8. Anthony Scaramucci, Mkurugnzi wa mawasiliano - 31 Julai 2017
  9. Reince Priebus, Afisa mkuu wa wafanyikazi wa umma - 28 Julai 2017
  10. Sean Spicer, Waziri wa habari - 21 July 2017
  11. James Comey, Mkurugenzi wa shirika la FBI - 9 Mei 2017
  12. Michael Flynn, Mshauri wa maswala ya usalama - 14 Februari 2017
  13. Sally Yates, acting attorney general - 31 January 2017
  14. Preet Bharara, New York federal prosecutor - 11 March 2017
  15. Paul Manafort, Trump campaign manager - 19 August 2016