TGNP Mtandao wakutanisha madiwani 20 kujadili kushirikiana

Zaidi ya madiwani 20, kutoka mikoa mitano na wilaya Nane wamekutana jijini Dar Es Salaam, kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao.

Madiwani hao ni kutoka Halmashauri za wilaya za Kishapu (Shinyanga), Tarime (Mara), Mbeya (Mbeya), Morogoro Vijijini (Morogoro) na manispaa za Ilala, Kinondoni na Ubungo (Dar es salaam).
Madiwani hao ambao walikutana katika ofisi za TGNP Mtandao, zilizopo Mabibo Dar Es Salaam, pia walipata nafasi ya kutembelea Kipunguni na kujionea mradi unaotekelezwa katika eneo hilo.
Pamoja na kujifunza masuala mbalimbali, Madiwani hao walipata fursa ya kushirikisha masuala ya kijinsia ambayo bajeti za Halmashauri zao zimezingatia na jinsi walivyofanikiwa kutenga rasilimali za kuhakikisha bajeti zao zinakidhi mahitaji ya kijinsia.
Wakiwa kata ya Kipunguni iliyopo manispaa ya Ilala madiwani hao walikutana na Diwani wa Kata hiyo na kujifunza jinsi ambavyo wananchi waliopo katika Kituo cha Taarifa na Maarifa walivyofanikiwa kuleta maendeleo kwa kushirikiana na viongozi ikiwepo kupambana na ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji.
Eneo hilo maarufu kwa wakazi wa kutoka mikoa ya kaskazini ambako yapo makabila yanayofanya ukeketaji nalo limekumbwa na tatizo hilo.
Aidha katika ziara hiyo, waheshimiwa madiwani walipata nafasi ya kujifunza, faida za mabunge ya jamii, na kujifunza miradi ya maendeleo ya kuwezesha wananchi kiuchumi ambayo inatekelezwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wananchi wa Kipunguni.
Katika mabadilishano ya uelewa mmoja wa wajumbe ambaye ni Diwani wa Ijombe wilayani Mbeya, Stimar Hepa John alisema kwamba wakati umefika kwa wananchi wengi kutambua shughuli za TGNP Mtandao.
Alisema awali alikuwa akidhani kwamba asasi hiyo ina mlengo wa kisiasa kiasi cha kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwao lakini baada ya elimu hii amebadili uelekeo na kuitaka taasisi hiyo kupeleka elimu Tanzania nzima.
Alisema, "Anaona kwamba TGNP ina jukumu kubwa nchini Tanzania na hivyo inastahili kuwa kila mahali kuwasaidia watanzania kujiimarisha katika nyanja zote."
Diwani huyo wa Ijombe ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Igawii alisema pamoja na kubadili mwelekeo aliwataka wabunge kuona kwamba wanapoandaa miradi hawaandai mbunge mpya bali kusaidia wananchi kujiinua kiuchumi.
Katika mkutano huo walitoa maazimio kadhaa ya kufanyiwa kazi katika halmashauri.
Miongoni mwa maazimio hayo ni namna ya kusimamia Mfuko wa Maendeleo wa wanawake kuhusu ile asilimia 5 na kutekeleza dhana ya viwanda.
Kwa mujibu wa Ofisa Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba mambo mengine waliyokubaliana ni kushawishi na kufuatilia ongezeko kila zahanati na vifaa vya kujifungulia na kuhimiza uwekaji wa mikakati ya kupambana na ukatili wa jinsia na kuunda kamati za ulinzi za mtoto.
Pia imeelezwa haja ya TGNP Mtandao kuendelea kutoa elimu kwa kusaidiwa na mabaraza ya halmashauri kuhusu rasilimali fedha na kufuatilia uwekezaji katika ujenzi wa hosteli kupunguza umbali wa watoto wa kike kutembea kufuata shule.
Mambo mengine ni kuona kwamba uandaazi wa bajeti unaanzia ngazi ya kijiji au mtaa badala ya kata na kukosekana kwa sauti za wananchi katika bajeti.
TGNP Mtandao ni asasi ya kiraia inayo fanya kazi na wanajamii kwa kipindi cha miaka 25 sasa, kwa kipindi chote hicho kimeshirikiana na taasisi za serikali, Wizara, Halmashauri na Kamati za Bunge za kisekta kwa ajili ya majadiliano, mashauriano na mafunzo ya namna ya kuboresha huduma za jamii kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Na Mwandishi wetu

Ofisa Programu uchechemuzi wa TGNP Mtandao, Deo Temba akifafanua jambo wakati akiendesha mjadala kwa Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8 walioshiriki mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.



Diwani wa Kata ya Songwa wilayani Kishapu, Shinyanga, Ngoromole Abdul akibadilishana uzoefu na madiwani wenzake wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.

Diwani wa Ijombe wilayani Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa shule ya sekondari Igawii, Stimar Hepa John akichangia kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.Diwani wa Kata ya Mshewe ya Wilaya ya Mbeya vijijini, mkoani Mbeya, Esther Mbega akishiriki kwenye mjadala wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.

Diwani wa Kata ya Ukenyenge ya wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Anderson Mandia akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni washiriki wakiendelea kujadiliana wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Madiwani 20 kutoka mikoa 5 na wilaya 8 walioshiriki mkutano wa kubadilishana uzoefu na kujifunza jinsi ya kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo katika kata zao uliondaliwa na TGNP Mtandao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hizo jijini Dar es Salaam.