Tokeo la picha la RAIS MAGUFULIWATANZANIA TUSIICHOKE AMANI
Na Emmanuel J. Shilatu
Misingi mizuri iliyojengwa na waasisi wa Taifa,
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume ,  imesababisha Wananchi wa
Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa amani na
utulivu, huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila ya kuingiliwa na mtu yeyote wa
ndani ama wa nje.

Tofauti na mataifa mengine, Watanzania wako huru
zaidi kwenda kokote wanakotaka na hata kuishi ama kufanya kazi au biashara bila
ya bughudha yeyote endapo taratibu na sheria za nchi zitafuatwa ama kuzingatiwa
vyema. Hali hiyo ni tofauti kabisa na nchi
nyingine zikiwamo zile za jirani zetu kama Kenya,
Rwanda, Burundi, Kongo na hata Uganda, nchi ambazo kwa kiasi kikubwa ukabila na
chokochoko za kisiasa zimetamalaki kuanzia ngazi za kijiji hadi Taifa. Hapa
kwetu tumeishi kamaNdugu bila ya u-rangi, udini,
ukabila wala harakati za kiitikadi na kisiasa kutugawa.
Jambo la kushangaza ni kuwa
misingi hiyo ya amani na utulivu
iliyogharamikiwa na Waasisi wetu, hivi sasa ipo shakani  na hatarini
kutoweka kwani ilishaanza kuchezewa na chokochoko za aina mpya ya siasa (kwa
maana ya ukosefu wa uvumilivu na uchu wa madaraka) iliyoanza kurindima katika
siku za hivi karibuni.
Kuna kundi dogo la watu ambao wanasema bila ya
woga, hofu wala aibu yeyote ile kuwa ni heri
kukosa amani kuliko kuishi maisha ya amani na utulivu bila ya kuheshimiwa. Na huku wengine
kwenye magari yao wakisadikiwa kuweka bango la maandishi makubwa
yanayosema ni heri ya vita inayofuata haki na
usawa kulikoamani inayopumbaza na kudhalilisha utu
wa Mwanadamu. Mbaya zaidi ni kuwa ujumbe huu
umekuwa ukipeperushwa karibu kila kona waendapo na magari yao. Hao ndio
Wanasiasa wetu.
Kinachoonekana hapa ni baadhi
ya wawania madaraka kutaka machafuko kutokana na uroho ama kasumba
ya  kuiga siasa za baadhi ya nchi ambazo hazijatulia huku wakijua
vyema hatma ya madhara yake yalivyo.
Kama si utahira basi ni utoto
kwa kufikiria dhana ya kheri ya kukosa amani ili
kupata heshima pasipo uchanganuzi wa fikra ya madhara yake ya kama si kuuawa ama kupata ulemavu endapo amani itatoweka. Pia, hiyo heshima wanayoitafuta itakuwa
na heshima gani endapo amani itayeyuka na vita
kutawala?

Hizi ni chokochoko
za kuchezea amani tuliyonayo, haina tofauti na
mtu achezeaye shilingi katikati ya kina cha bahari. Inavyoonekana watu hawa
wamesahau ule msemo wa wahenga “ usione vyaelea, ujue vimeundwa”;
wanafikiria amani tuliyonayo imeletwa na Mungu
kutoka mbinguni bila ya uwepo wa wajenzi wa amani .
Hawajiulizi, kwanini nchi za Rwanda, Burundi, Kongo walifikia kwenye hatua ya
kupigana wenyewe kwa wenyewe. Je, ni kwamba
Mungu hawawapendi (ila anatupenda sisi tu) hadi akaruhusu hali ya vita kutokea?
Tusijidanganye, wajenga amani ni Wazawa
wenyewe.
Tangu mwaka huu uanze tumeuanza kwa masikio na
macho yetu kupokea yale ambayo hatukuwahi kuyazoea maishani mwetu. Ni ajabu sana lakini ni kweli
ya Watanzania tumefikia hatua ya raia wake kutaka kupima nguvu na vyombo vya
dola, Hii haijawahi kutokea.
Leo hii si kaskazini, kusini, mashariki wala
Magharibi kote huko kumejaa vumbi linaloashiria kuichoka amani tuliyonayo.
Tatizo kubwa tulilonalo hapa ni kuruhusu siasa
na Wanasiasa kutuburuza pasipo sie kuwa ndio waongozaji wa maisha yetu binafsi.
Katika siku za hivi karibuni kumetokea mijadala
mikali sana ya juu ya sakata la maandamano linalochochewa kupitia mitandao ya
kijamii huku yakichagizwa na Wanasiasa, Wanaharakati na Watu wengineo wasio na
uchungu na Taifa letu la Tanzania.
Tumesikia kauli mbalimbali nzito toka kwa vyombo
vya dola pamoja na viongozi wa Kitaifa. Tumemsikia IGP, Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama Nchini, tumemsikia Waziri wa Mambo ya Ndani na kama haitoshi
tumesikia kauli nzito toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.
John Pombe Joseph Magufuli akitoa angalizo, onyo, tahadhari juu ya wale wote
waliopanga kuandamana kuwa wasifanye hivyo yasije yakawakuta makubwa.
Ndugu zangu, Kuna Mwanamapinduzi mmoja wa
Burkina Faso aitwaye Hayati, Kapteni Thomas Sankara. Kijana huyu aliacha hiba
njema ya kuenziwa ndani ya nchi yake, Afrika na duniani.
Katika kauli zake Sankara alipata kukaririwa
akisema; “Ningependa kuacha nyuma yangu, imani ya kuwa, kama tunaimarisha
kiwango fulani cha uangalifu na oganaizesheni, basi, tunastahili ushindi. Kamwe
huwezi kuleta mabadiliko ya kimsingi bila ya kuwa na kiwango fulani cha
uwendawazimu”.
Mara nyingi chochezi za sampuli hii (ya kufanya
maandamano unaofanywa mitandaoni), wanaoathirika ni Wananchi
wa kawaida yaani mimi na wewe, wanyonge na walalahoi tusio na kimbilio zaidi ya
kugeuzwa madaraja na mitaji kwao, na maumivu kwetu.
Historia inajidhihirisha kuwa nchi zilizotokea
machafuko, tumeshuhudia wanaoshabikia ndio huwa chambo na wa kwanza kukumbwa na
madhara ya kujeruhiwa, kuuawa ama mali zao kuharibiwa vibaya. Hata siku moja
haijawahi kutokea wachochezi ama viongozi hao kuwa ni waathirika
katika kile wanachowahamasisha watu wakifanye.
Tuchukulie kwa mfano mauaji ya kimbari ya Rwanda
ya mwaka 1994 ama machafuko yaliyowahi kutokea Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa
mwaka 2007, mamia kama si maellfu ya watu (wananchi
wa kawaida) walijeruhiwa, wengine kupoteza maisha yao huku mali zao
zikiharibiwa vibaya mno.
Lakini hakuna kiongozi wa chama angalau wa ngazi
ya wilaya, tuliyemsikia akipata madhara yeyote yale. Viongozi wote
walioshinikiza hali hizo kutokea walikuwa nchi za nje na si Afrika tena wakila
kuku kwa mrija wao, wake na watoto zao.
Kwa upande wa Kenya, baada ya hali kutulia, huku
watu wakiishi kwenye mahema na misiba kila kona ikirindima, walijitokeza (wale
wale wachochezi) kutoa pole kwa waliouawa, kuumia au kupoteza mali na Wapendwa
wao. Kama haitoshi wakaamua kuwang’ong’a kama si kuwakebehi kwa kuwaita mashujaa, kisha viongozi
hao wakaendelea na shughuli za kisiasa na baadhi yao ni wakubwa
serikalini mpaka kesho. Wale wananchi wa kawaida wameambulia sifa na shukrani
za kikebehi yenye majuto tele.
Nadhani umejionea ni  jinsi
gani ambavyo wananchi wa kawaida wanavyoathirika pindi machafuko
yanapotokea. Ni vyema Wananchi na wazalendo
wote wa Taifa hili, kukataa nguvu yeyote ile ya uchochezi, iliyo na mapandikizi
ya chuki,  na wanaotaka kutugawa kwa nguvu na akili zetu zote.
Historia inadhihirisha kuwa ni rahisi
sana kuchochea machafuko, lakini ni ngumu sana
kulitoa Taifa katika machafuko hayo, ni jambo
linaweza kuchukua miaka na miaka katika kupata ufumbuzi wake na vyema sana
Watanzania kutokuichoka amani tuliyonayo.
Ndugu zangu, hatuna sababu ya kuanza kuonyeshana
misuli ya nani anaweza kumwoa binti Fulani wakati bado yu tumboni mwa Mama
yake. Kwa kufanya hivyo niwazi tunavidhulumu vizazi
vijavyo ambao wao haswaa ndio wenye gesi yao na wao ndio wajenzi wa Taifa la
baadae.
Inawezekana kabisa miaka zaidi ya 50 tuliyoishi
kwa amani na utulivu imewapumbaza baadhi ya
Watu na kuanza kufikiria maisha ya Taifa la Mapigano ambayo siye hatujayazoea.
Ndugu zangu, Wapo wanaosema kuwa amani ni sawa na yai mkononi, ukilivunja hautaweza kuliunganisha kamwe;
wengine wanasema kuwa amani haina bei na
ikipotea haina soko la kununua. Tuitunze amani yetu
na kamwe tusiizoee wala kuichoka!
Mungu Ibariki Tanzania.
0767488622