Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi pamoja na mkuu wa wilaya hiyo Joseph Mkudew wakielekea eneo ambalo kituo cha afya kinajengwa kwa ajili ya kwenda kufanya ukaguzi na kupokea maelezo ya ujenzi huo na namna pesa za serikali katika sekta ya afya zinavyotumika.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi   pamoja na viongozi wengine wa wilaya hiyo wakiwa kwenye eneo ambalo kituo hicho kinajengwa.
 Mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitenda wakati wa ziara ya waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
ya ukaguzi miradi ya afya na kujua namna gani pesa
zilizotolewa na serikali zinavyotumika katika halmashauri ya wilaya ya Ileje

Na Fredy Mgunda,Ileje

Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
amefanya ziara ya ukaguzi
miradi ya afya na kujua namna gani pesa
zilizotolewa na serikali zinavyotumika katika halmashauri ya wilaya ya Ileje
mkoani Songwe.
 

Akiwa katika zira hiyo,Waziri Mwalimu
alifanikiwa kukagua kituo cha afya cha Lubanda ambacho kilipewa kiasi cha shilingi
milioni mia tano(500)  kutoka serikalini
kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya kwa wananchi wa halmashauri hiyo.



“Mimi nimekuja kuangalia
utekelezaji wa pesa ambazo serikali tunazileta huku kwa kwa ajili ya kuboresha
sekta ya afya,maana kumekuwa na watendaji ambao wamekuwa wakizitumia vibaya pesa
ambazo tumekuwa tukizileta huku” alisema  Waziri Mwalimu



Waziri Mwalimu alisema kuwa
ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa kituo cha afya cha Lubada unaoendelea kwa
kasi nzuri na kwa viwango ambavyo serikali inavitaka na kuahidi kuwa ukimalika
ujenzi huo utawaletea gari la kubebea wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya kuokoa
maisha ya watanzania.



“Kwa hapa mlipofikia
nawapongeza sana kwa kuwa kazi nimeiona kwa macho yangu mwenyewe hivyo
mkimaliza ujenzi nitakikisha kila kitu kinachotakiwa hapa kitakuwepo ili
kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa wilaya ya Ileje” alisema Waziri Mwalimu



Hata Waziri Mwalimu aliupongeza
uongozi wa halmashauri ya Ileje kwa kufikisha asilimia tisini na moja (91) ya
wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambao unarahisisha
upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa wananchi wanaotumia mfuko huo.



“Niwapongeze tena kwa kazi
kubwa mliyofika ya wananchi wengi kukubali kujiunga kwenye mfuko huo,maana kuna
halmashauri nyingine zijafgika hata robo yenu hiyo naona utendaji wenu
uliotukuka katika kuwatumikia wananchi wa Ileje” alisema Waziri Mwalimu



Waziri Mwalimu alizitaka
halmashauri nyingine kuiga mfano wa halmashauri ya ileje kwa namna wanavyofanya
kazi kwa ushirikiano mkubwa baina ya mkurungezi mtendaji na mkuu wa wilaya hiyo
ndio maana kuna matokeo chanya.



“Nichuke nafasi hii kukupongeza
sana mkurugezi wangu Haji Mnasi na mkuu wa wilaya Joseph Mkude kwa ushirikiano
mnaoushesha katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa wilaya ya Ileje,napenda
kama halmashauri zote hapa nchini zingekuwa kama halmashauri yetu tungekuwa
tumefika mbali kimaendeleo” alisema Waziri Mwalimu



Awali akisoma hotuba kwa
waziri, mkurugenzi wa halmashuri hiyo Haji Mnasi alisema kuwa halmashauri
imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wananchi wote wanajiunga na mfuko wa afya ya
jamii  kwa kutoa elimu juu ya umuhimu wa
kujiunga kwenye mfuko huo.



“Tunasheria ya mwaka 2004 ambayo
inawataka wananchi wote wajiunge kwenye mfuko huo hivyo tutaitumia vizuri
sheria hiyo kuhakikisha kuwa kila mwananchi anajiunga kwenye mfuko huo akiwa
tayari amepatiwa elimu ya kutosha na kumfanya ajiunge mwenyewe bila
kulazimishwa” alisema Mnasi



Mnasi alisema kuwa huduma za
matibabu kwa wazee zinatolewa katika vituo vyote 33 vya huduma za afya na jumla
ya wazee 11463 waliotambuliwa na walipewa vitambulisho ni 8954 sawa na asilimia
78 ambapo jumla ya shilingi 7,196,000 zilitumika mwaka 2016/2017 kwa ajili ya
kutoa huduma kwa wazee.



“Lakini ukiangalia mwaka
2017/2018 tumetenga kiasi cha shilingi 28,000,000/= ambapo kwa kila zahanati
tunapeleka kiasi cha shilingi 1,000,000 na kwenye vituo vya afya tunapeleka
2,000,000 kwa ajili ya huduma ya wazee na kazi ya kuendelea kuwatambua ni
endelevu” alisema Mnasi





Mnasi alimuahidi Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kuwa
pesa zote zinazoletwa kutoka kwenye wizara yake zitatumika kama zilivyopangwa
na kuhakikisha zinasimamiwa vizuri kama ambavyo wamekuwa wakisimamia pesa zote
za serikali zitumike kwa malengo yanayokusudiwa.