Pichani kuanzia Kushoto kwenda Kulia ni Charles Kie, Mkurugenzi Mtendaji wa, Ecobank Nigeria Ltd; Serigne Dioum, Mtendaji wa MTN’s , Hudma za kifedha kwa njia ya mtandao; Ade Ayeyemi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa, Ecobank Transnational Incorporated (ETI), Rob Shuter, Ofisa Mtendaji mkuu wa MTN na Patrick Akinwuntan, Mtendaji wa  Ecobank Transnational Incorporated (ETI)
Na Mwandishi wetu

KAMPUNI ya simu MTN imeingia ubia na moja ya benki inayoongoza barani Afrika ya Ecobank Transnational Incorporated (ETI) kuwezesha  wateja wao kufaidika na huduma za kifedha zinazotolewa na makampuni hayo.
Imeelezwa kuwa MTN ikijivunia idadi kubwa ya wateja wanaotumia huduma zake mbalimbali; mtandao mkubwa wenye uhakika; bidhaa zenye ubunifu na huduma zake za kifedha kwa mtandao imeungana na Ecobank kuwezesha wateja wao kuanzisha kufungua akaunti na kupitisha miamala yao kupitia mtandao wa MTN.
Makampuni hayo mawili maarufu barani Afrika yametiliana saini mkataba wa makubaliano utakaowezesha kushirikiana katika kubuni na kuwezesha huduma za kifedha zenye ubora wa kiwango cha juu kati ya benki hiyo na mtandao wa simu wa MTN.
Miongoni mwa huduma zitakazotolewa ni kuwezesha miamala mbalimbali kufanyika kwa kutumia simu na akaunti za benki.
Kutumia mitaji iliyopo katika uwekezaji ndani ya  Ecobank na MTN kuwezesha miamala ya kimataifa kufanyika kidigitali.
Aidha makubaliano hayo yatachochea ubunifu wa bidhaa mbalimbali katika upande wa hifadhi ya fedha kwa njia ya mtandao na ukopeshaji wake na kutoa nafasi ya malipo kwa njia ya mtandao kwa wateja, wafanyabiashara na mashirika mbalimbali.
Ade Ayeyemi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ecobank anasema: “ Mabadiliko ya kidigitali katika mifumo ya benki na simu kunatengeneza fursa za namna bora ya kuwezesha kutoa huduma za kifedha. Afrika  inalazimika kwenda mbio katika digiti ili kuwezesha fursa zilizopo zitumike kuwatumikia wateja. MTN na  Ecobank leo wamechukua hatua kubwa kuwezesha fursa hizo” .
Pia alisema kwamba  mkakati wa benk hiyo wa kidigiti kwa muda mrefuj umelenga kuhakikisha nafuu ya uwezeshaji wa miamala katika soko.
Akizungumzia ushirikiano huo Ofisa Mtendaji Mkuu na Rais, Rob Shuter alisema: “Ushirikiano kati ya mabenki na watoaji wa huduma za miamala kwa njia ya simu ni muhimu, hivyo uhusiano wetu wa muda mrefu  na Ecobank umelenga kuwezesha huduma za fedha kuwafikia wananchi wengi na kwa urahisi zaidi. Tumefurahishwa na  maafikiano haya kwani yametupeleka hatua nyingine, kwani ushirikiano wetu utawezesha ubunifu utakaowezesha huduma za fedha kupenya kila mahali katika bara hili.”