Dola za Marekani milioni 210 ziliibwa na wadukuzi kutoka kwenye Benki na Taasisi za serikali nchini Kenya mwaka 2017.
Hii ni kwa mujibu w ripoti ya shirika la usalama mitandaoni, SERIANU, ambayo inasema mataifa ya bara la Afrika yalipoteza jumla ya dola milioni 350.

Ikizingatiwa kwamba, kati ya mwezi Januari na mwezi Februari mwaka jana, Kenya ilipoteza dola milioni 50 kwa wadukuzi, ni wazi kwamba usalama wa fedha za wateja wa benki haujazingatiwa na benki nyingi.
"Udukuzi ni uhalifu unaobadilika kila kunapokucha" anasema Delano Kiilu, mtaalamu wa masuala ya usalama mitandaoni.
Kutoka kushoto: Mkurugenzi mkuu wa Serianu limited William Makatiani, waziri wa ulinzi wa Kenya balozi Raychel Omamo na kaimu mkurugenzi mkuu wa maamlaka ya mawasiliano habari na technolojia nchini Kenya wakati wa uzinduzi wa ripoti ya usalama mitandaoni mwaka 2007, April 10, 2018.Haki miliki ya pichaSERIANU
Image captionKutoka kushoto: Mkurugenzi mkuu wa Serianu Limited, William Makatiani, Waziri wa Ulinzi wa Kenya, Balozi Raychel Omamo na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano, Habari na Teknolojia nchini Kenya wakati wa uzinduzi wa ripoti ya usalama mitandaoni mwaka 2007, Aprili 10, 2018.

Je, benki zimeshindwa kulinda pesa?

Kulingana na Delano, benki nyingi nchini Kenya zimejiandaa vya kutosha kulinda pesa na maelezo ya wateja wake kikamilifu.
Hata hivyo wadukuzi wanaonekana kuwa wabinifu na kila siku wanapata mbinu mpya za kuiba pesa.
"Benki nyingi zinawekeza katika mbinu za usalama za kulinda dhidi ya mbinu za wizi wa zamani, na hawana uwezo wa kujikinga dhidi ya wizi wa kesho" anasema Delano Kiilu.
Hata hivyo mwanauchumi Ali Khan Sachu anatofautiana na msimamo huo na anashikilia kuwa benki za kitaifa nchini Kenya hazijawekeza vya kutosha katika usalama mifumo ya usalama mitandaoni.
"Hii ni gharama ya kufanya biashara, na ndio sababu benki nyingi zinatoza riba ya kiwango cha juu ili kufunika hasara kama hiyo ya udukuzi" Anasema bwana Sachu.
Aidha ukosefu wa sheria thabiti za kulinda habari za Wakenya mitandaoni unachangia kahatarisha usiri wa wateja kwenye banki.
Delano Kiilu
Image captionDelano Kiilu

Wizi huu unatokea vipi?

Kila siku wadukuzi wanabuni njia mpya za kudukua mifumo ya usalama mitandaoni huku benki zikisalia nyuma hatua moja.
Kulingana na bwana Delano, 70% ya udukuzi unafanikishwa na wafanyikazi kwenye benki pamoja na wateja.
30% unatokana na wadukuzi kugundua mianya kwenye mifumo ya usalama kwenye banki.
Wadukuzi wengi wanatumia mbinu tofauti ikiwemo, kutuma ujumbe wa barua pepe unaowavutia wafanyakazi , na wanapofungua wanawezesha wadukuzi kupenya kwenye mitandao ya benki hizo.
"wafanyakazi wanatoa maelezo muhimu na ya siri kwa wadukuzi na kurahisisha wizi huo unagundulika muda mrefu baada ya kufanyika". Anasema bwana Delano.
Mwanamme aliyevalia kofia akifanya kazi kweny tarakilishi.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWadukuzi wamekuwa kero kubwa ulimwenguni.
Baadhi ya wadukuzi wanaiba kiasi kikubwa cha pesa kwa mpigo, huku wengine wakiiba kiasi kidogo cha pesa

Mbona benki nyingi haziripoti wizi huo?

Benki nyingi zinaogopa kupoteza wateja iwapo zitatangaza hadharani kwamba zimeshindwa kulinda pesa na maelezo ya wateja.
Hofu kubwa inatokana na wateja kujiondoa mara moja kwa wingi na kusababisha benki kufungwa.
Wizi wa maelezo na pesa unatokea bila wateja kujuzwa, na maelezo hayo yanatumika dhidi ya wamiliki wake.
"Nadhani wakati umefika kwa benki kuwafahamisha wateja wake kuhusu upungufu uliopo kwenye mifumo ya usalama na kufafanua jinsi wanavyokabiliana na tatizo hilo". Anasema bwana Ali Khan Sachu.

Je, biashara za mitandaoni zinajikinga vipi?

Bara la Afrika limeshuhudia ongezeko kubwa la biashara za mitandaoni.
Waafrika wengi wanatumia mitandao kununua bidhaa, lakini je, usalama wa maelezo yao binafsi umehakikishwa?
Fredrick Kirui mkurugenzi mkuu wa mtandao wa kibiashara Afrika Sokoni
Image captionFredrick Kirui mkurugenzi mkuu wa mtandao wa kibiashara Afrika Sokoni
Kulingana na Fredrick Kirui, mkurugenzi mkuu wa mtandao wa mauzo mitandaoni AfrikaSokoni, maelezo binafsi ya wateja sio salama.
"Mitandao mingi kimataifa na hususan barani Afrika inakabiliwa na changamoto ya wadukuzi wanaobobea kila siku". Anasema bwana Kirui.
Bwana Kirui hata hivyo anawataka wateja kuwa waangalifiu wakati wananunua bidhaa mitandaoni ama wanapopeana habari binafsi kwa kampuni za mitandaoni, kwani maelezo hayo yanatumika kuwaibia pesa na pia kuwashawishi mitandaoni.
Bwana Kirui anahoji kwamba unapotoa maelezo yoyoyte unafaa kuuliza iwapo kweli yanahitajika.