Barbara Bush, mke wa Rais Mstaafu wa Marekani, George H. W. Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.
Barbara, pamoja na kuwa mke wa Rais, alikuwa mama wa Rais mstaafu wa Marekani, George Walker Bush. Anakubukwa kwa mchango wake wa kufuta ujinga ndani ya familia pale alipoanzisha mfuko wa kusaidia kaya masikini kujua kusoma na kuandika.
Alikuwa 'first lady' tangu 1989 hadi 1993. Mapema wiki hii, Barbara aliripotiwa kuwa hali yake ni mbaya na madaktari walikuwa wamefikia hatua ya mwisho ya kumtibu. Mtoto wake, George Bush, amenukuliwa na BBC akisema kuwa familia yao inasikitika kupoteza mama ambaye alikuwa mcheshi na kuongeza "alikuwa na bahati kuwa na mama kama Barbara."
0 Comments